KOMPYUTA ZAIBWA HALMASHAURI YA HAI

0
479

Na Safina Sarwatt, Hai

WATUMISHI wa watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kuvunjwa kwa moja ya ofisi zao na kuibwa kompyuta sita.

Kwa mujibu wa Kamanda  wa Polisi Mkoa wa  Kilimanjaro, Hamisi Issah, wizi huo ulitokea Juni 27 mwaka huu  saa tano asubuhi huku akidai kuwa tukio hilo limegubikwa na utata mkubwa ndani yake.

“Taarifa iliyoripotiwa katika ofisi yangu ni jumla ya kompyuta mpakato tatu aina Dell  ambazo thamani yake ni Sh milion 12, tukio hilo limegubikwa na utata mkubwa ndani yake hivyo tunaendelea kuwahoji watumishi hao,”alisema Kamanda.

Alisema kuwa ofisi hiyo iliyovunjwa ni ya kuhifadhi kumbukumbu za vizazi na vifo na kwamba mpaka sasa ripoti iliyotolewa polisi ni kuibiwa kwa kompyuta mpakato tatu tu.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,  Yohana Sintoo alikiri kuibwa kwa vifaa hivo.

“Kweli ofisi  ya NIDA ilivunjwa juzi usiku wa kuamkia jana, wezi hao waliingia na kuchukua kompyuta sita tu ambazo zilikuwa zinatumika kuhifadhia kumbukumbu nakuacha,”alisema Sintoo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here