33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kombora la kisasa Urusi laanza kazi, lashtumiwa

MOSCOW, Urusi

KOMBORA la kwanza lenye teknolojia ya kisasa la Avangard Hypersonic, limeanza kufanya kazi, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema.

Hawakusema ni wapi kombora hilo lilifanyiwa majaribio,maofisa awali walisema litarushwa katika milima ya Urals.

Rais Vladimir Putin wa Urusi, alisema  kombora hilo lenye uwezo wa kinyuklia, lina kasi ya mara 20 ya sauti na linaiweka Urusi mbele ya mataifa mengine.

Marekani imelifanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri

 Lina “mfumo wa glide” ambao unarahisisha usafiri wake na linaweza kuwa vigumu kujilinda dhidi yake

Waziri wa Ulinzi, Sergei Shoigu alithibitisha kombora la “Avangard hypersonic glide liliianza kufanyakazi saa 10:00 za Moscow Desemba 27 na kuliita “tukio muhimu”.

Rais Putin alisema mfumo wa Avangard, unaweza kupenya mifumo ya ulinzi ya makombora ya kisasa na ile ya baadaye na kuongeza: “Hakuna hata nchi moja inayomiliki silaha kama hiyo mbali na ile ya masafa marefu inayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.”

Mataifa ya magharibi na mataifa mengine yalikuwa “yakicheza nasi”, alisema.

Alizindua silaha hiyo na mifumo mingine ya silaha katika hotuba yake ya kitaifa mnamo Machi, mwaka jana.

Desemba mwaka jana,silaha hiyo iligonga lengo la mazoezi ya umbali wa kilomita 6,000 (maili 3,700) katika uzinduzi wa jaribio lililofanyika kambi ya makombora kusini mwa milima ya Urals.

Silaha hiyo, haiwezi kutunguliwa na mfumo wowote wa ulinzi wa adui, alisema Rais Putin bada ya jaribio hilo.

Likiwa juu ya kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine , silaha ya Avangard inaweza kubeba silaha ya kinyuklia ilio na uzani wa hadi megatani mbili.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi, ilitoa video ya mfumo wa Avangard, lakini wataalamu wa silaha wameelezea kutilia shaka ufanisi wake.

Katika taarifa, Pentagon ilisema “haitapinga madai ya Urusi” juu ya uwezo wa Avangard. Marekani ina mpango wake wa kombora la mfumo wa Hypersonic, kama ilivyo China, ambayo  2014, ilisema ilifanya majaribio ya silaha kama hiyo.

Novemba 26, mwaka huu, Urusi iliruhusu wataalamu wa Marekani kukagua kombora la Avangard chini ya sheria za makubaliano mapya ya 2010, azimio linalolenga kupunguza idadi ya silaha za kimkakati za kinyuklia .

Makubaliano hayo ambayo yataisha mnamo februari 2021, ni makubaliano makubwa ya mwisho ya kudhibiti silaha za nyuklia kati ya Urusi na Marekani.

Agosti, mwaka huu, Marekani ilijitoa katika Mkataba wa Vikosi vya Nyuklia (INF) ambao ulitiwa saini na Rais wa Marekani, Ronald Reagan na kiongozi wa Soviet, Mikhail Gorbachev mwaka1987.

Rais wa Marekani, Donald Trump alisema anataka mkataba mpya wa kinyuklia kutiwa saini na Urusi  na China.

Ni vigumu kubaini iwapo mfumo mpya wa kombora la Urusi la Avangard umeanza kufanya kazi, kama inavyodaiwa na Moscow, au ni majaribio yake tu.

Lakini hamu ya Rais Putin kutaka kujivunia kwa kiwango fulani, inahesabiwa kuwa haki yake. Urusi inaonekana kupiga hatua kubwa katika ujenzi wa makombora hayo ya kisasa. . China pia inaendeleza mifumo kama hiiyo wakati Marekani inaonekana kusalia nyuma kidogo.

Makombora ya mhemko, kama linavyomaanisha jina lake huruka kwa haraka sana, yaani lina kasi ya angalau mara tano ya ile ya sauti.

Yanaweza kuwa makombora ya aina ya cruise, yanayowezeshwa wakati wote wa urushaji wake. Au yanaweza kubebwa juu ya kombora la masafa marefu ambalo hujitawanya na kuendelea kuelekea katika lengo lake kwa kasi ya juu.

Ikiwa madai ya Urusi ni ya kweli, huenda imeanzisha mfumo wa kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambalo litakuwa vigumu kujilinda dhidi yake

Tangazo  kombora hilo la Avangard limeanza kufanya kazi linazua enzi mpya na hatari katika ushindani wa kutengenza silaha za kinyuklia

Inathibitisha kwa mara nyingine mtazamo wa Rais Putin juu ya kusisitiza na kurasimisha silaha za nyuklia.

Hoja ya Marekani,ni mipango yake ya kujilinda na makombora dhidi ya mataifa yasioaminika kama vile Iran, Korea Kaskazini imepuuziliwa mbali na Urusi.

Yote haya yanajiri wakati ambapo mtandao mzima wa makubaliano ya kudhibiti silaha kutoka kwa vita baridi yanaporomoka .

Mkataba mmoja muhimu – Mkataba mpya wa Start – unatarajiwa kumalizika mnamo Februari 2021. .

Pamoja na kizazi kipya cha silaha za nyuklia, wengi wanaamini sio tu mikataba iliyopo inapaswa kusitishwa, lakini mikataba mipya inahitajika kusimamia kinachoweza kugeuka kuwa ushindani mpya wa silaha za nyuklia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles