26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Koffi Olomide kufanya shoo ya Selfie leo Dar

4129894293_e64ddfb827_bNA CHRISTOPHER MSEKENA

WAKATI mwanamuziki mkongwe katika muziki wa dansi anayetokea Congo, Koffi Olomide akitarajiwa kufanya onyesho la nguvu leo usiku, mmiliki na mwanamuziki wa bendi ya Malaika, Christian Bella, amewataka wasanii wawe makini kufuatilia onyesho lake ili wajifunze kitu kutoka kwa mwanamuziki huyo.

Christian Bella alisema wasanii wanatakiwa kuiga na kujifunza namna ya utumbuizaji na siri ya kuendelea kudumu kwenye muziki kwa muda mrefu kwa mkongwe huyo anayetarajiwa kufanya onyesho lake leo viwanja vya Escape One Mikocheni katika onyesho linaloitwa Selfie 16 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 16 ya kituo cha redio Clouds Fm tangu kilipoanzishwa.

Christian Bella alisema mkongo huyo huwa habahatishi katika maonyesho yake ndiyo maana amewataka wasanii waige namna anavyofanya akiwa stejini na namna anavyoweza kudumu katika muziki akiwa na mashabiki lukuki.

“Unajua ukizungumzia wasanii wakubwa Afrika, Koffie ni mmojawapo, watu wanashangaa kwanini mkongwe huyo hachuji kwenye soko la muziki, sasa siri hiyo wasanii wa Bongo inatakiwa tumuulize na kufuatilia onyesho lake vizuri ili tujifunze mengi kutoka kwake,” alisema Bella.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles