24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Kodak Black kumbe alikuwa anapigwa sana jela

NEW YORK, MAREKANI 

STAA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Bill Kapri, maarufu kwa jina la Kodak Black, ameanika jinsi alivyokuwa anapigwa wakati yupo jela.

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 22, kwa sasa yupo huru baada ya kutoka jela kutokana na kesi ya kumiliki silaha bila kibali na kujihusisha na dawa za kulevya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo amedai alikuwa mmoja kati ya watu ambao wamepigwa kwenye jela ya Kentucky.

“Kuna siku nilipigwa na askali saba wa jela, wakati wananipiga walikuwa wananiambia, nikiwa mtaani ninaonekana staa sana na nina kundi kubwa la watu nyuma yangu, lakini gerezani siwezi kuwa staa, hivyo ninaweza kupata mateso kama wengine, walisema hayo huku wakinipiga,” aliandika rapa huyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles