24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha wa England Gareth Southgate Ajiuzulu Baada ya Kichapo cha Euro 2024

London, Uingereza

Kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate, amejiuzulu siku mbili baada ya kushindwa na Hispania kwenye fainali ya Euro 2024.

England ilifungwa 2-1 mjini Berlin Jumapili, kikiwa ni kipigo chao cha pili mfululizo katika fainali ya Euro, baada ya kuchapwa kwa penalti na Italia kwenye Uwanja wa Wembley miaka mitatu iliyopita.

Southgate, mwenye umri wa miaka 53, aliiongoza timu ya taifa katika michezo 102 ndani ya kipindi cha miaka minane ya uongozi wake.

Mkataba wake ulikuwa unamalizika baadaye mwaka huu. “Kama Muingereza wa kujivunia, imekuwa heshima katika maisha yangu kuichezea Uingereza na kuinoa England,” alisema Southgate.

“Imekuwa na maana kwa kila kitu kwangu, na nimetoa yangu yote. Lakini ni wakati wa mabadiliko, na sura mpya.”

Mtendaji Mkuu wa Chama cha Soka, Mark Bullingham, amesema mchakato wa kumteua mrithi wa Southgate umeanza na “Tunalenga kuwa na meneja mpya haraka iwezekanavyo,” amesema.

Aliongeza kuwa FA “ina suluhu la muda iwapo litahitajika” na hatatoa maoni zaidi kuhusu mchakato huo hadi bosi mpya atakapoteuliwa.

Mechi inayofuata ya England ni dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika Ligi ya Mataifa ya Ulaya mnamo Septemba 7.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles