29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Kocha Stars aeleza ya moyoni

CHARLES-BONIFACE-MKWASAEVANCE KIGANJA Na DOREEN PANGANI-(TUDARCO)

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Mkwasa, ametoa ya moyoni akidai kikosi chake kilikumbwa na matatizo mengi ndani na nje ya uwanja ambayo yalichangia kufungwa bao 1-0 na Nigeria katika mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon).

Stars iliyopangwa Kundi G kwenye michuano hiyo pamoja na Misri waliofuzu kucheza fainali hizo zitakazofanyika nchini Gabon, ilimaliza hatua ya makundi ikiwa nafasi ya mwisho kwa kuambulia pointi moja.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkwasa alisema tatizo kubwa lilijitokeza pale wachezaji walipokosa jezi za kubadilisha na kulazimika kuingia uwanjani kipindi cha pili wakiwa wameloana kutokana na kusafiri na jezi moja moja, jambo ambalo hakulifurahia.

Alisema sababu nyingine iliyochangia kupata kipigo dhidi ya Nigeria ilitokana na wachezaji kukosa muda wa kutosha kufanya maandalizi, kwani walifanya mazoezi kwa muda wa siku mbili ambao hautoshi kuleta matokeo  mazuri.

“Tulifanya maandalizi ya muda mfupi sana wakati tulikuwa tunakwenda kucheza na kikosi imara cha Nigeria chenye wachezaji wenye majina na wazoefu,” alisema Mkwasa.

Kocha huyo pia alielezea kutofurahishwa na kitendo walichofanyiwa na Shirika la Ndege la Ethiopian  ambalo lilishindwa kuwatafutia wachezaji sehemu ya kulala, jambo ambalo lilichangia kuwaondoa hamasa ya mchezo.

“Wachezaji hawakujisikia vizuri kwani kitendo walichofanyiwa hakikuwa cha kiungwana, hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa kuwahoji kujua kwani nini hali hiyo ilijitokeza,” alisema Mkwasa.

Aidha, Mkwasa alisema hawezi kumpa adhabu yoyote beki wa Yanga, Kelvin Yondani, ambaye aligoma kujiunga na timu hiyo kwa madai kuwa kama hayupo tayari kuichezea timu hiyo atatafuta mchezaji mwingine wa kuziba nafasi yake.

“Mchezaji anayeitwa kuichezea timu ya Taifa, anatakiwa kuwa mzalendo, hivyo siwezi kumlazimisha kama hayupo tayari,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles