25.5 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Kocha Singida United awatupia lawama wachezaji wake

Theresia Gasper-Dar es Salaam

KOCHA Mkuu wa Singida United, Ramadhan Nsanzurwimo, amewatupia lawama wachezaji wake kwa kushindwa kufanya kile alichowaelekeza na kukubali kichapo cha mabao 3-1, dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Liti Singida.

Singida United juzi ilizimwa tena baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mchezo huo na kuruhusu mabao mengi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Nsanzurwimo alisema wachezaji walitoka mchezoni na kuwapa nafasi wapinzani wao ya kupata mabao ya mapema.

“Wachezaji wangu walicheza tofauti na kile nilichowaelekeza, hivyo walitoka mchezoni tangu mwanzo, wanakuja kurudi badae kwenye fomu na mechi inaisha,” alisema.

Alisema kwa sasa ataenda kuyafanyia kazi mapungufu hayo ili yasijitokeze kwa mara nyingine katika mechi zinazowakabili mbele yao.

Kocha huyo alisema makosa mengine yalifanywa na mabeki wake ambao waliruhusu mabao kirahisi hivyo katika kipindi hiki atawaweka sawa kabla ya kucheza mchezo mwingine.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles