27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Kocha Simba: Nataka ubingwa wa jasho

Na WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

WAKATI wadau wa soka nchini wana mtazamo tofauti kuhusu mustakabali wa Ligi Kuu Tanzania Bara baadhi wakitaka Simba itangazwe bingwa na wengine wakitaka lisubiriwe janga na corona lipite michezo yote imalizike, kocha wa Wekundu hao, Sven Vanderbroeck amesema anautaka ubingwa alioupigania hadi mwisho.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimama baada ya Serikali kupiga marufuku kwa siku 30 shughuli zinazosababisha mikusanyiko ikiwemo michezo, ikiwa ni tahadhari ya kuepuka kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona.

Marufuku hiyo ilianza Machi 17 mwaka huu na itafikia tamati Aprili 17.

Hata hivyo baada ya siku 30 za katazo la Serikali kukamilika, kuruhusiwa au kutoruhusiwa kuendelea kwa shughuli za mikusanyiko ikiwemo michezo kutategemea na hali ya ugonjwa huo itakavyokuwa.

Lakini kuna wasiwasi huenda Serikali ikaongeza siku zaidi kutokana na idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa huo hapa  nchini kuongezeka, hivyo kutishia afya za Watanzania.

Sven alifunguka msimamo wake huo jana wakati alijibu maswali ya wadau wa soka nchini kupitia mitandao ya kijamii ya Klabu ya Simba.

Shabiki mmoja aliuliza kama angependa amalize ligi hadi mwisho au akabidhiwe ubingwa.

Akijibu swali hilo kocha huyo alijibu anapenda kumalizia mechi 10 zilizobaki na kukabidhwa taji lake.

“Ningependa kucheza hadi mechi ya mwisho na kukabidhiwa ubingwa nikiwa nimemaliza mechi zote za ligi, kuliko kupewa na uongozi wa shirikisho,” alisema Sven.

Kuhusu usajili

Kocha huyo alisema hana mpango wa kupangua kikosi chake, badala yake anapenda kuendelea kufanya kazi na wachezaji wote alionao kikosini kwa sasa kwakua wana viwango vya juu.

Aliseleza kuwa kama ni kusajili sehemu anayofikiria kuongeza mchezaji ni ulinzi na kiungo ili kuongeza idadi ya wachezaji waliopo katika nafasi hizo.

“Bado nina kikosi kizuri na ninatamani kuendelea na kila mchezaji aliyepo, mawinga wapo wa kutosha, kama nitaongeza ni kiungo mmoja na walinzi wawili,” alisema Sven.

Ndemla kusugua benchi

Akizungumzia wachezaji wawili wa kikosi hicho ambao mashabiki wanatamani kuwaona uwanjani, Said Ndemla na Yusup Mlipili, alisema kusugua kwao benchi kutokana na ushindani uliopo katika nafasi wanazocheza.

Alisema soka linahitaji mtu aliyefiti, imara na vitu vya ziada, hivyo anavyopanga kikosi anaandangalia  anayefaa kwa wakati muafaka.

“Ndemla ni mchezaji mzuri, anajua kutumia vizuri mguu wa kulia, anapiga pasi ndefu vizuri, lakini  anahitaji kuwa vifi zaidi kutokana na uwepo wa Clatous Chama na  viungo wengine.

“Mlipili naye hivyo hivyo na nimeshamueleza mara nyingi kitu anachotakiwa kufanya, kikosi ni kipana na kila mchezaji ni nzuri, linapokuja suala la kuchagua nani acheze unangalia yule aliyefanya vizuri mazoezini,” alisema.

Ataja mechi ngumu

Sven alisema miongoni mwa wapinzani wake aliokutana nao msimu huu, michezo dhidi ya timu za Yanga, JKT Tanzania na Lipuli ilikuwa migumu zaidi kwao.

Alisema JKT walimsumbua kutokana na kuwa na safu imara ya ulinzi ambayo ni ngumu kupenya.

“Mechi nyingine iliyokuwa ngumu kwangi ni ile ya Lipuli, tulicheza ugenini halafu katika hali ambayo si nzuri kutokana na mvua iliyonyesha siku hiyo,” alisema.

Katika michezo hiyo yote, Simba ilifungwa na  JKT iliifunga bao 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru na kushinda bao 1-0 dhidi ya Lipuli.

Changamoto

Alisema awali alipata changamoto akiwa kama kiongozi wa benchi la ufundi kutokana na lugha pamoja na kutozoea mazingira, hali iliyompa wakati mgumu na kuonekana haelewani na wenzake.

Lakini baada ya kukaa pamoja na kuelewa vizuri soka la Tanzania, aliweza kushirikiana na watu wote wa benchi la ufundi na kupanga mikakati mbalimbali.

“Sasa hivi tunafanya kazi pamoja kama bechi la ufundi, tunashirikiana vizuri, haikuwa rahisi, ukiliangalia sasa utaona tunashirikiana sana na hata ukiangalia moja ya picha iliyopigwa na mtu wetu wa habari ni kwamba kila kitu kinafanyika vizuri,” alisema Sven.

Amsubiri Miraji kwa hamu

Alisema mshambuliaji wake Miraji Athumani ni kati ya wachezaji anaowategemea katika kufunga mabao, hivyo uwepo wake unamfanya asiwe na mpango wa kusajili straika mwingine.

Alieleza kuwa kuna kipindi alilazimika kutumia mshambuliaji mmoja kutokana na nyota huyo pamoja  na John Bocco kuwa majeruhi, lakini hali yake imeanza kuimarika atarejea uwanjani.

“Nafikiri safu yangu ya ushambuliaji itakuwa vizuri zaidi, Miraji  kwa kuwa Miraji ameanza mazoezi ni mchezaji mwenye mchango mkubwa,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles