28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Kocha Simba: Ajib, Kahata habari nyingine

Theresia Gasper – Dar es Salaam

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameshindwa kuzuia hisia zake na kumpongeza kiungo wa timu hiyo, Ibrahim Ajib, akisema ndiye chachu ya ushindi wao dhidi ya Polisi Tanzania.

Simba juzi iliendeleza ubabe katika mechi za Ligi Kuu, msimu huu, baada ya kuinyuka Polisi Tanzania mabao 2-1, mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Wekundu hao walilazimika kusubiri hadi kipindi cha pili ili kupata mabao yao, baada ya Polisi kutangulia kufunga la kuongoza kipindi cha kwanza.

Mashujaa wa Simba kwenye mchezo huo walikuwa mshambuliaji John Bocco, aliyefunga bao la kusawazisha na Ajib ambaye alikwamisha la ushindi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, VandenBroeck, alisema katika mechi mbili mfululizo kikosi chake kimeonekana kuchoka zaidi kipindi cha pili licha ya kupata matokeo ya ushindi.

“Tulianza kwa kasi ya chini lakini mabadiliko niliyofanya ya kumuingiza Ajib yalileta mabadiliko ikiwa pamoja na kiwango cha  Francins Kahata kiliweza kuleta presha kwa wapinzani wetu,” alisema.

Alisema ataendelea kuongeza nguvu zaidi kwenye kikosi chake kwani anahitaji kila mchezaji aweze kuonyesha uwezo na kuleta matokeo.

VandenBroeck alisema kuna makosa ambayo ameyaona katika timu yake hivyo watayafanyia kazi kabla ya mchezo unaofuata kwani asingependa yajirudie kwa mara nyingine.

Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kupambana ili waweze kupata ushindi mnono kwenye mechi zinazofuata,  ukizingatia wapinzani  pia wamejipanga.

Simba imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 50, baada ya kucheza mechi 19, ikishinda 16 , sare mbili na kupoteza mmoja.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles