27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Senegal: Bila Mane Stars watalala

CAIRO, MISRI

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Senegal, Aliou Cisse, ameweka wazi kuwa, kumkosa mshambuliaji wao Sadio Mane katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri sio tatizo kubwa la kuwakabili Taifa Stars.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atakosa mchezo wa kwanza wa kundi C dhidi ya Tanzania, Juni 23 kutokana na kuoneshwa kadi mbili za njano katika michezo ya mwisho ya kufuzu kushiriki michuano hiyo.

”Kutokuwpo kwake hakutatuathiri kwa njia yoyote, ukweli ni kwamba uwepo wake ni muhimu sana kwetu lakini bila yeye tuko vizuri kupambana na Tanzania, Shirikisho la soka CAF limeamua hivyo basi hatuna budi,” alisema kocha huyo. 

Mane alipewa kadi ya njano katika mechi ambayo Senegal ilipata ushindi wa bao1-0 dhidi ya Equitorial Guinea, Novemba 17, 2018, pia alipokea kadi nyengine ya njano katika mechi ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Madagascar, Machi 23, 2019.

Michuano hiyo nchini Misri, itaanza Juni 21 hadi Julai 19, hii itakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo kukosa mchezo wa ufunguzi. 

Mara ya kwanza alikosa mchezo wa ufunguzi wa Simba hao wa Teranga katika fainali za 2015 nchini Equitorial Guinea dhidi ya Ghana kwa kuwa alikuwa anauguza jeraha la kifundo cha mguu alilopata alipokuwa akiichezea klabu yake ya zamani Southampton. 

Mane amekuwa kwenye kiwango kizuri misimu miwili iliopita akiwa na klabu yake ya Liverpool, msimu uliomalizika hivi karibuni amemaliza Ligi huku akiwa mfungaji bora wa Ligi England, akiwa na jumla ya mabao 22 sawa na wapinzani wao Mohamed Salah na Piere Aubameyang.

Hata hivyo Mane alikuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha Liverpool kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2017/2018 na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo katika msimu wa 2018/2019.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles