27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha England amkingia kifua Wayne Rooney

roonry

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa muda wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate, amemkingia kifua nahodha wa timu hiyo, Wayne Rooney, baada ya mashabiki kumzomea mchezaji huyo.

England juzi ilifanikiwa kushinda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Wembley dhidi ya Malta, huku Rooney akichezeshwa katika nafasi ya kiungo, lakini mashabiki walionekana kutokubaliana na kiwango cha mchezaji huyo.

Mchezaji huyo amekuwa akibadilishwa namba mara kwa mara, awali alikuwa anacheza katika nafasi ya ushambuliaji, lakini kocha wa zamani wa Manchester United, Van Gaal, alianza kumchezesha katika nafasi ya kiungo ambapo hadi sasa amekuwa akicheza nafasi hiyo katika baadhi ya michezo.

Tangu ujio wa kocha mpya, Jose Mourinho, ndani ya kikosi hicho, amekuwa akicheza kwa kusuasua kutokana na ushindani wa namba, hivyo kumfanya aonekane kiwango chake kimeshuka.

Hali hiyo imewafanya mashabiki wa timu ya taifa ya England kutumia mitandao ya kijamii na kumwomba astaafu soka la timu ya taifa na nguvu zake azipeleke katika klabu yake.

Katika mchezo wa juzi wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia, Rooney alipewa nafasi ya kucheza katika safu ya kiungo, huku akiwa na Jordan Henderson, timu hiyo ilifanikiwa kushinda mabao mawili ambayo yalifungwa na Daniel Sturridge na Dele Alli, lakini mashabiki walimzomea Rooney.

Kocha wa England, Southgate, ambaye amechukua nafasi ya Sam Allardyce, amewashangaa mashabiki kumzomea Rooney katika mchezo huo.

“Sielewi kwanini mashabiki wanamzomea Rooney, sijui walikuwa wanatarajia kuona nini kutoka kwa mchezaji huyo, lakini wanasahau alichokifanya Rooney ndani ya timu hii.

“Mashabiki wanatakiwa kuangalia enzi za John Terry, Frank Lampard, Ashley Cole na wingine, katika kipindi chao England ilikuwa inabaguliwa juu ya wachezaji hao, lakini ukiangalia michezo waliocheza pamoja na mataji waliochukua ni mengi.

“Rooney ni mchezaji wa kujivunia ndani ya England, ninaamini muda utafika mchezaji huyo ataweza kuondoka kama ilivyo kwa wachezaji wengine,” alisema Southgate.

Hata hivyo, Rooney aliwahi kusema kuwa hata kama kiwango chake kimeshuka, lakini atahakikisha anarudi katika ubora wake ili aweze kuitumikia England katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles