26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Azam aipania Ndanda

Stewart-HallNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA wa timu ya Azam, Stewart Hall, amesema atahakikisha kikosi chake kinapata ushindi dhidi ya Ndanda ya Mtwara kesho baada ya kuambulia pointi moja dhidi ya Yanga Jumamosi iliyopita.

Hall aliyepania kushinda mechi kumi za kwanza za Ligi Kuu, amesema mechi dhidi ya Yanga imevuruga hesabu zake, lakini ameyafanyia kazi makosa yaliyowagharimu ili kuendeleza wimbi la ushindi.

Azam ambayo msimu uliopita ilifungwa bao 1-0 na timu hiyo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara kesho, imepania kuvunja mwiko kwa kuwachapa Ndanda, ambapo mpaka sasa imejikusanyia pointi 16 kwenye mechi sita walizocheza.

“Tulidhamiria kushinda mechi zetu zote kumi za kwanza, lakini Yanga wametuvurugia kwa kupata sare. Lakini bado hatujaharibikiwa sana, tutapigana kuhakikisha tunashinda mechi zinazofuata tukianzia Mtwara dhidi ya Ndanda.

“Nashukuru wachezaji wangu wanatambua majukumu yao, hivyo tunachokifanya sasa ni mazoezi ya kawaida kuelekea kwenye mchezo huo,” alisema.

Azam itaondoka kuelekea mkoani humo leo saa 5 asubuhi mara baada ya mazoezi.

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles