RIO DE JANEIRO, BRAZIL
BAADA ya mwanamieleka, Mandakhnaran Ganzorig, kushindwa katika fainali za michuano ya Olimpiki nchini Brazil, makocha wa mchezaji huyo waliamua kuvua nguo kwa kupinga matokeo hayo.
Fainali hizo ambazo zilifikia mwisho juzi, Ganzorig alishuka dimbani kupambana na mpinzani wake, Ikhtiyor Navruzov, lakini alijikuta akipoteza pambano hilo kwa alama 7-6, lenye uzito wa Kg 65.
Kutokana na hali hiyo, makocha wa mwanamieleka huyo, Byambarenchin Bayaraa na Tsenrenbataar Tsostbayar, walijikuta wakivua nguo kwa kupinga ushindi wa mpinzani wao na kudai kuwa waamuzi hawakutenda haki kwa kuwa zilibaki sekunde 10 kumalizika kwa mchezo huo.
“Huu ni uonevu, waamuzi wa mchezo hawakuwa makini na kile ambacho walikuwa wanakifanya, ukweli ni kwamba mchezo huo uliisha kabla ya muda kukamilika.
“Mamilioni ya watu wa bara la Asia walikuwa wanangoja kuona mshiriki wao akirudi na medali ya shaba, lakini kutokana na kile ambacho waamuzi wamekifanya, mambo yamekwenda tofauti na tumeshindwa kufanya hivyo.
“Kwa hali ya kawaida tulistahili kuondoka na ushindi, lakini kulikuwa na mambo ambayo yameendelea kinyume na taratibu sahihi,” alisema Bayaraa