27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

KMC yafungashiwa virago Caf

Theresia Gasper -Dar es salaam

TIMU ya KMC imeondolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya jana kuchapwa mabao 2-1 na AS Kigali ya Rwanda, mchezo wa marudiano uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza kati ya timu hizo ulichezwa Agosti 10, jijini Kigali  na kumalizika kwa suluhu.

Matokeo hayo yaliufanya mchezo wa marudiano kuwa mgumu kwa kila timu, kwani kila moja ilikuwa inahitaji ushindi ili kusonga mbele.

Wageni ndio waliokuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 29, kupitia kwa mshambuliaji Rashid Kalisa.

Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika.

Kipindi cha pili, KMC inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni iliingia na nguvu zaidi ya kutaka kusawazisha nap engine kuongeza jingine, lakini ilijikuta ikifungwa bao la pili dakika ya Erick Nsabimana,  baada ya mabeki wake kujichanganya walipokuwa wakitaka kuweka mtego wa kuotea.

Licha ya kufungwa bao hilo, KMC haikukata  tamaa, badala yeka iliendeleza mapambano na kufanikiwa kupata bao dakika ya 87, kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Suleiman Ndikumana.

Pamoja na kosa kosa nyingi za washambuliaji wa KMC, Salim Aiyee na Ndikumana, dakika 90 za pambano hilo zilikamilika kwa AS Kigali kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha wa KMC, Jackson Mayanja alisema kikosi chake kilicheza vizuri, lakini kilishindwa kupata matokeo mazuri kutokana na uzoefu mdogo katika michuano ya kimataifa hususan Kombe la Shirikisho ambayo walikuwa wanashiriki kwa mara ya kwanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,406FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles