26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

KMC wataja siri ya chapa chapa yao

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa KMC, umetaja  siri ya kikosi chao kufanya vizuri katika michezo yake mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kuwa ni wachezaji kujituma na kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

KMC inaiongoza msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi tisa, baada ya kupata ushindi kwenye michezo yake yote mitatu iliyoshuka dimbani.

Timu hiyo inayomilikiwa na Manispaa ya Kindononi katika Jiji la Dar es Sa laam, ilizindua msimu kwa kishindi baada ya kuilaza Mbeya City mabao 4-0, ikailaza Tanzania Prisons mabao 2-1(michezo yote ikichezwa Uwanja wa Uhuri, Dar es Salaam) kabla ya kuitungua Mwadui mabao 2-1, Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Akizungumza na MTANZANIA, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa kila mchezaji wao anatambua majukumu yake na kutimiza kwa wakati jambo linalowapa matokeo chanya.

“Wachezaji wanatambua kwamba nini kinahitajika ndani ya timu na wao hesabu zao ni kuona wanapata ushindi hiyo ndiyo furaha yao pia.

“Kwa kufanya hivyo kunawafanya wawe na nguvu katika kupambana na kupata matokeo na hicho ndicho ambacho kinatokea, tupo na tunazidi kupambana zaidi na zaidi,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles