31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Klopp: Nahitaji pointi 105 kunyakuwa ubingwa EPL

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Liverpool, Jurgen Klopp, anaamini kikosi chake kinahitaji kuweka rekodi kwa kufikisha pointi 105 kuipiku timu ya Manchester City na  kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Kauli hiyo inakuja baada ya juzi usiku Liverpool kuifunga Wolves mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Molineux, huku mabao ya timu hiyo yakifungwa na Mohamed Salah na Virgil van Dijk.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu  England ikiwa na  pointi 48 katika michezo 18 iliyocheza bila kuruhusu kupoteza mchezo wowote hadi sasa.

Manchester City ambayo ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, itapishana pointi moja na Liverpool iwapo itashinda mchezo dhidi ya Crystal Palace ambao ulitarajiwa kuchezwa jana Uwanja wa Etihad.

Kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi, kunaifanya Liverpool kuwa katika hali nzuri kushinda taji la Ligi Kuu msimu huu.

Lakini Klopp amewaeleza wachezaji wake kuwa wasiridhike licha ya kuwa na pointi nyingi msimu huu.

Manchester City msimu uliopita ilinyakuwa taji hilo ikiwa na rekodi ya kufikisha pointi 100 na Klopp anaamini anatakiwa kupata zaidi ya hizo ili kufikia lengo msimu huu.

“Kama tunataka kufanya kweli tunatakiwa kufikisha pointi 105.

“Sifahamu kiasi gani cha pointi ambazo timu nyingine zinahitaji kupata katika msimu huu, lakini kila mmoja anazungumza kuhusu nafasi yetu kwamba mara nne timu zilizokaa kileleni sikukuu ya Krismasi zilitwaa ubingwa.

“Lakini lazima tujiulize kuhusu ushindani, kulingana na pointi walizonazo washindani wetu.

“Msimu huu unaonekana kuwa maalumu kwetu maana kuwa na pointi 48 kipindi hiki si kitu kidogo, mwisho wa msimu unatakiwa kuwa na pointi 105 ili kuwa bingwa,” alisema Klopp.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles