29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Klopp hataki kumuona Balotelli Liverpool

Jurgen Klopp
Jurgen Klopp

LIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA mpya wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp, alimwondoa mshambuliaji wa klabu hiyo, Mario Balotelli, katika kikosi ambacho kilicheza dhidi ya Tranmere na amedai kwamba hana mpango wa kumpa nafasi kwenye kikosi chake.

Timu hiyo kwa sasa ipo katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano mbalimbali nchini England, hivyo Klopp amedai kwamba hakuwa na mipango yoyote na mchezaji hiyo hata katika michezo ya kirafiki.

Inasemekana kwamba kocha huyo alifanya mazungumzo na mchezaji huyo na kumtaka atafute timu ya kuitumikia kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.

“Tangu Balotelli ajiunge na mazoezi ya klabu hii Julai 2, ameonekana kuwa na tabia nzuri na siwezi kusema kama alikuwa na tofauti na sisi.

“Nilikuwa na wasiwasi katika ujio wake kwamba angeweza kufanya mambo tofauti, lakini ukweli ni kwamba hakuna tofauti yoyote.

“Uwezo wake wa zamani umekuwa tofauti na sasa, najua kama ana kipaji kizuri lakini uwezo huo alionao kwa sasa hawezi kushindana namba na wachezaji waliopo hapa.

“Kwa upande wangu nitahakikisha ninamuweka katika ubora wake ili aweze kupata nafasi ya kucheza soka sehemu nyingine, ninaamini hii si sehemu yake sahihi kwa sasa, nitafanya mazungumzo juu ya hilo maana hapa hana tena nafasi.

“Kwenye namba ambayo yeye anataka kucheza ina wachezaji wenye uwezo mkubwa kama vile Daniel Sturridge, Christian Benteke, Divock Origi na Danny Ings, itakuwa ngumu kuwanyang’anya namba wachezaji hao,” alisema Klopp.

Mchezaji huyo alijiunga na klabu ya AC Milan kwa mkopo msimu uliopita, hata hivyo alidai kwamba hana mpango wa kurudi nchini England kwa kuwa maisha ya Italia ni mazuri zaidi.

Klabu ya Sampdoria imesema ina nia ya kumsajili mchezaji huyo ambaye ameonesha kiwango kidogo msimu uliopita katika klabu ya AC Milan.

Balotelli alijiunga na klabu ya Liverpool mwaka 2014 kwa kitita cha pauni milioni 16 akitokea AC Milan, kabla ya kurudi tena msimu uliopita kwa mkopo. Mchezaji huyo kwa sasa analipwa kitita cha pauni 90,000 kwa wiki ndani ya kikosi hicho.

Ndoto za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ni kuja kuwa bora duniani na kutwaa tuzo ya uchezaji bora wa dunia wa Ballon d’Or na amesema hawezi kukata tamaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles