24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Klopp amwacha beki wake Mamadou Sakho

Jurgen Klopp na Sakho

LIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp, ameamua kuachana na beki wake wa kati, Mamadou Sakho, katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu nchini England na michuano mbalimbali.

Mchezaji huyo alisimamishwa kushiriki soka kutokana na kashfa ya kutumia dawa za kusisimua misuli, lakini baada ya uchunguzi, nyota huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa ameonekana kuwa huru kurudi michezoni.

Hata hivyo, mchezaji huyo ni majeruhi, anasumbuliwa na enka ambayo aliipata mwishoni mwa msimu uliopita wa ligi kuu na kuna uwezekano mkubwa wa kukosa michezo ya awali ya msimu mpya kutokana na hali hiyo.

Kutokana na hali hiyo, kocha huyo wa Liverpool, Klopp, ameamua kuachana na mchezaji huyo katika kikosi chake kilichoelekea California nchini Marekani, kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Hali ya mchezaji huyo inadaiwa kuwa vizuri lakini inasemekana ana tatizo lingine la nidhamu hivyo kuna uwezekano Klopp amemuacha mchezaji huyo kutokana na nidhamu yake kuwa mbaya.

Hata hivyo, hali hiyo inaweza kumfanya mchezaji huyo asiwe na nafasi tena ndani ya kikosi hicho japokuwa anaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Liverpool.

Mchezaji huyo amekuwa nje ya uwanja tangu kumalizika kwa ligi kuu nchini England, pia aliachwa katika kikosi cha timu ya taifa katika michuano ya Euro 2016, huku Ufaransa wakiwa wenyeji wa michuano hiyo na kushindwa kuchukua ubingwa dhidi ya Ureno.

Bado klabu ya Liverpool ina tatizo la beki, huku baadhi ya mabeki wake kama vile Kolo Toure akiwa tayari amejiunga na klabu ya Celtic, Martin Skrtel naye amejiunga na klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki.

Liverpool inatarajia kucheza na Chelsea mchezo wa Kombe la ICC, kesho kutwa, Julai 31 watacheza na AC Milan, katika kombe hilo, Agosti 2, watacheza na Roma, wakati huo Agosti 6 watapambana na Barcelona na Agosti 7, watacheza na Mainz.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles