33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Klopp ahofia Liverpool kuondolewa Uefa

LIVERPOOOL, ENGLAND

BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Napoli, kocha wa timu hiyo Jurgen Klopp, ameweka wazi kuwa, wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo wa mwisho kuweza kufuzu hatua inayofuata.

Katika kundi lao E, wanaongoza wakiwa na pointi 10, huku Napoli wakiwa na pointi 9 na Red Bull wakiwa na pointi saba.

Mchezo unaofuata ambao utaamua timu mbili kuingia hatua ya 16 bora, Liverpool watakutana na Red Bull ambao wamekuwa kwenye ubora wa hali ya juu msimu huu, hivyo mabingwa hao watetezi wanahofia kuupoteza.

Kwa upande mwingine Napoli mchezo unaofuata watakuwa nyumbani na kuwakaribisha Genk, hivyo wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo, endapo watafanikiwa kushinda basi watakuwa na pointi 12, wakati huo Red Bull wakishinda watakuwa na pointi 10 sawa na Liverpool, hivyo watakuwa wanaangalia timu yenye mabao mengi ya kufunga.

Hivyo kitu ambacho Liverpool wanakiangalia kwenye mchezo huo ni kushinda au kutoa sare, lakini wakifungwa basi safari yao ya kutetea ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya itakuwa imefikia mwisho.

“Sare kwa Napoli ina maana kubwa kwao, wanadhani tayari wamefanikiwa kuingia hatua inayofuata na kweli inawezekana wakafanya hivyo, lakini kwa upande wetu kila mmoja anasema Mungu wangu! Itakuwa ngumu kufuzu, kweli itakuwa ngumu sana,” alisema kocha huyo.

Klopp aliongeza kwa kusema atapambana kuhakikisha anashinda mchezo huo bila ya kujali ubora wa wapinzani wao, “Tunatakiwa kushinda mchezo huo, bila shaka tunatakiwa kumaliza nafasi ya kwanza kwenye hatua ya makundi, tunaamini inawezekana hata kama kila timu kati ya Napoli na Red Bull zinataka nazo kushinda michezo yao ya mwisho,” aliongeza kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles