22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

KKKT yamsimika Dk. Mbilu kuwa Askofu kamili wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

Na Amina Omary, Tanga

Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki imepata kiongozi wake baada ya kusimikwa rasmi Dk. Mch. Msafiri Mbilu kuwa Askofu kamili.

Askofu Dk. Msafiri Mbilu amesimikwa rasmi kuwa Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki baada ya baada ya kufanyika misa rasmi hii leo katika Siku ya Bwana ya 5 baada ya PASAKA.

Mwezi November 25-26,2020,ulifanyika uchaguzi wa kumtafuta Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na ndipo Dk. Msafiri Mbilu kuteuliwa kuwa Askofu mteule wa Dayosisi hiyo.

Misa hiyo ya kumsimika Uaskofu imeongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Dkt.Fedrick Shoo katika Kanisa Kuu la Lushoto,mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Dk. Mbilu anakua Askofu wa awamu ya Tano katika Dayosisi ya Kaskazini Mashariki tangu kuanzishwa na msaidizi wake akiwa ni Michael Kanju.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles