30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa tuhuma za kuiba Tanzanite ya Sh milioni 200

JANETH MUSHI-ARUSHA

MKAZI wa eneo la Lemara jijini Arusha, Joel Kazimoto (26), amepandishwa kizimbani akikabiliwa na makosa manne ya wizi ikiwemo ya madini aina ya Tanzanite yenye thamani ya Sh milioni 200 na fedha tasilim Sh milioni 81.

Mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, mtuhumiwa huyo alipandishwa kizimbani jana ambapo Jamhuri iliwakilishwa na wakili  Ahmed Khatibu, utetezi ukiwakilishwa na wakili Edmund Ngemela.

Akimsomea mashitaka hayo katika kesi hiyo ya jinai namba 87 ya mwaka huu, Wakili Khatibu alidai kosa la kwanza mtuhumiwa anadaiwa kati ya Juni Mosi mwaka jana na Juni 30 ,eneo la Njiro aliiba madini hayo ambayo ni mali ya Emanuel Wado.

Kosa la pili anadaiwa Desemba 23 mwaka jana eneo la Njiro aliiba fedha tasilimu Sh milioni sita mali ya Frida Emanuel.

Kosa la tatu anadaiwa tarehe isiyojulikana kati ya mwaka 2018 hadi 2019, eneo la Njiro aliiba fedha taslimu Sh milioni 60, mali ya Emanuel Wado.

Wakili huyo alidai kosa la nne mtuhumiwa huyo anadaiwa kati ya mwaka 2018/2019 eneo la Njiro, aliiba Dola za Marekani 7,000 ambazo zilikuwa sawa na Sh milioni 15 mali ya Emanuel Wado.

Mshitakiwa huyo alikana kutenda makosa hayo ambapo Wakili Khatibu alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa kwa shauri hilo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Jeniffer Edward,manayesikiliza shauri hilo alimweleza mshitakiwa huyo dhamana iko wazi kwa masharti ya kuweka Sh milioni 140 kwenye akaunti ya mahakama au kuwasilisha hati ya mali iliyothaminiwa yenye thamani hiyo.

“Kwa sasa hivi masharti yaliyotolewa mteja wangu hataweza kutekeleza, amekaa mahabusu polisi zaidi ya siku 45 kabla ya kuletwa mahakamani, naomba muda ili mteja wangu atimize mashsrti aliyopewa,”alisema Wakili Ngemela

Hakimu Jeniffer aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 16 mwaka huu, ambapo mshitakiwa huyo alipelekwa mahabusu ya Gereza Kuu la Kisongo kwa kushindwa kutumiza masharti ya dhamana yaliyotolewa na mahakama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles