31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kumsukuma mtoto kwenye karai la mafuta

law-1

Na JOHANES RESPICHUS, DAR ES SALAAM

MKAZI wa Msasani Bonde la Mpunga, Doreen Swedi (35), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kutuhumiwa kumsukuma mtoto Husna Hamis kwenye karai la mafuta ya moto na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Mbele ya Hakimu Obadia Bwegoge, Wakili wa Serikali, Nancy Mushumbusi, alidai kwamba tukio hilo lilitokea Septemba 29, mwaka huu huko Msasani.

“Mtuhumiwa unadaiwa kwamba ulimsukuma Husna kwenye karai hilo lililokuwa na mafuta ya moto na aliungua sehemu mbalimbali za mwili hivyo kumsababishia maumivu makali wakati ukitambua ni kinyume cha sheria,” alidai  Mushumbushi.

Baada ya maelezo hayo mtuhumiwa alikana kufanya kosa hilo na Mushumbushi alidai upelelezi bado haujakamilika hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Hakimu Bwegoge alisema kwa mujibu wa sheria shtaka hilo linadhaminika hivyo alimtaka mtuhumiwa kuja na mdhamini mmoja wa kuaminika atakayeweka saini ya maandishi katika bondi ya Sh milioni tatu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 17, mwaka huu na mtuhumiwa alidhaminiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles