27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa kumkashifu Rais

JPMM

MANENO SELANYIKA NA PAULINA KEBAKI (TUDARCO)

MHASIBU wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kilichopo Dar es Salaam, Elizabeth Asenga (40), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mtandao wa kijamii.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, Wakili wa Serikali, Leonard Chalo, alidai mahakamani hapo kwamba mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 6, mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa kutuma ujumbe wa kashfa dhidi ya rais katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Wakili Chalo alidai kuwa mshtakiwa alituma ujumbe huo kwenye kundi la wanamtandao wa whatsup liitwalo stj staff Social group.

Aliyakariri mahakamani maandishi ya kashfa yaliyoandikwa na Elizabeth kuwa; ‘Hakuna Rais kilaza kama huyu wetu duniani. Angalia anavyompa Lissu umashuhuri, fala lile picha yake ukiweka ofisini nuksi tupu ukiamka asubuhi ukikutana na picha yake ya kwanza usiku inakuwa ni mkosi mwanzo mwisho.’

Mshtakiwa alikana shtaka lake na kutakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa Serikali au taasisi yoyote inayotambulika kisheria ambao walitakiwa kuwasilisha mahakamani barua kutoka kwa waajiri na vitambulisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles