KIZIMBANI KWA KULAWITI MTOTO WA MIAKA 12

0
635

b897c623

JOHANES RESPICHIUS Na ATUPENDA GEOFREY (MPS)-DAR ES SALAAM

MKAZI wa Tandale Kinondoni, Dar es Salaam, Ramadhani Ibrahim (32), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12 (jina tunalo).

Akisomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi, Boniface Lihamwike, Mwendesha Mashtaka, Tumaini Mfikwa, alidai mtuhumiwa alifanya kosa hilo Novemba 18, mwaka jana maeneo ya Tandale.

“Novemba 18, mwaka jana, maeneo ya Tandale, mtuhumiwa Ramadhani kwa makusudi ulimlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12, huku ukijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria,” alidai Mfikwa.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na kuambiwa shtaka hilo linadhaminika awe na wadhamini wawili ambao walitakiwa kusaini bondi ya Sh 2.5.

Kesi hiyo, iliahirishwa hadi Januari 23, mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo kwa kusikilizwa kwa mara ya kwanza na mtuhumiwa alirudishwa rumande kutokana na kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here