25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Kizimbani kwa kukutwa na dawa za kulevya

 GODFREY SHAURI Na BATROMAYO JAMES (DSJ) -DAR ES SALAAM

WAKAZI wa Mwananyamala kwa Kopa Furaha Hassan (35), na Ester Albet (41) wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi Kinondoni kujibu shtaka la kukamatwa na madawa ya kulevya.

Watuhumiwa hao walikana kutenda kosa hilo huku upande wa jamhuri ulisema upelelezi wa shauri hilo limekamilika.

Awali akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Rehema Mwaisaka, Wakili wa Serikali Violeth David alidai mnamo septemba 12 mwaka 2017 watuhumiwa walikamatwa na madawa ya kulevya ainaya (Heroin) yenye uzito wa 15.26g maeneo ya Mwananyamala

Hata hivyo upande wa Jamhuri ulisema upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba tarehe ya kusomwa tena kwa shauri hilo.

Hakimu Mwaisaka alisema kesi hiyo ina dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waamifu, wawe wafanyakazi wa serikari, wawe na vitambulisho vya Taifa pamoja na barua kutoka serikari za mitaa.

 Mshtakiwa wa kwanza Furaha alikidhi vigezo vya dhamana na kuachiwa, mshitakiwa wa pili Ester alishindwa kutimiza masharti ya dhamana baada ya mdhamini wake kushindwa kueleza vyema uhusiano wao. 

Hivyo mtuhumiwa huyo alirudishwa rumande hadi atakapokidhi vigezo vya dhamana.

Kwa upande wa Jamhuri ulisema kesi hiyo itakuja kusomwa tena Machi 19, mwaka huu.

Wakati huo huo mkazi wa wa kigogo Mbuyuni Rashidi Abdallah (19) na Hamisi Abubakari (19), mkazi wa kigogo kati walipandishwa kizimbani kwa tuhuma ya unyang’anyaji wa simu. 

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu John Chacha, wakili Veronica Mtafya alidai kuwa mnamo Desemba 31, mwaka 2019 walimnyang’anya Abubakari Mohamedi simu aina ya Tecno yenye thamani ya Sh 220,000 huku wakiwa na silaha aina ya panga.

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo huku upande wa jamuhuri ulisema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kutoa tarehe kwa ajili ya hukumu.

Hakimu Chacha alisema kesi hiyo haina dhamana hivyo washtakiwa watarudishwa rumande hadi machi 19 mwaka huu hukumu itakapotolewa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles