23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

KIZIMBANI KWA KUJIFANYA MWANAMKE NA KUOLEWA

NA FLORENCE SANAWA – MTWARA

 

MWANAUME mmoja, Sharafi Issa, maarufu Zamda Salum (19), mkazi wa Kijiji cha Milango minne, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara kwa kosa la kujifanya mwanamke na kufunga ndoa na mwanaume mwenzake kisha kuishi naye nyumba moja kama mume na mke.

Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Richard Kabate na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali, George Makasi.

Kabate alidai kuwa kitendo hicho cha watu wenye jinsia moja ya kiume kuishi nyumba moja kama mke na mume ni utovu wa kimaadili na ni kinyume na kifungu 157 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 sheria iliyofanyiwa marekebisho ya mwaka 2002.

Alidai kuwa mshtakiwa Sharafi alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti mwezi Machi na Juni, mwaka huu katika vijiji vya Mkahala na Mpanyani ndani ya Halmashauri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara, kwamba kwa makusudi katika jamii, alijifanya mwanamke na kumshawishi Mustara Nurudin Saidi kwa kumtongoza na kufunga naye ndoa isiyo halali.

Baada ya mshtakiwa huyo kusomewa shitaka hilo linalomkabili, alikana na Wakili Makasi aliiambia mahakama kuwa upelelezi bado haujakamilika.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles