Kizimbani kwa kesi ya kubaka

0
471

ERICK MUGISHA NA PATRICIA KOMBA (SAUT)DAR ES SALAAM

Mkazi wa ubungo maziwa Salum Lumanyika (24) amepandishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kinondoni kwa kosa la ubakaji.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Esther Mwakalinga na mwendesha mashtaka wa jamuhuri, Ellen Masulali alidai Mei mosi mwaka huu, katima eneo la ubungo maziwa jijini Dar es salaam alimbaka binti wa miaka 23.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka hilo mbele ya mahakama na mwendesha mashtaka wa serikali alidai upelelezi bado hauja kamilika ambapo aliomba kesi itajwe tarehe nyingine.

Hakimu mwakalinga alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, barua za utambulisho na nakala ya vitambulisho vya taifa.

Hata hivyo mshtakiwa amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi yake itatajwa tena Oktoba 16 mwaka huu.

Wakati huo huo watu watatu wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kinondoni kwa kosa la kukutwa na bangi gramu 86.75.

Watuhumiwa hao ni Ramadhani Emmanuel (28) mkazi wa ubungo, Ziko William (30) mkazi wa ubungo maziwa na Innocent Edward (17) mkazi wa ubungo maziwa.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya hakimu Happiness Kikoga na wakili wa serikali Ester chale alidai Agosti 23 mwaka huu, eneo la ubungo wilayani ubungo jijini Dar es salaam walikutwa na majani yaliyokatazwa kinyume na sheria aina ya bangi kiasi cha gramu 86.75.

Washtakiwa wote walikana kutenda shtaka hilo mbele ya mahakama na wakili wa seriakali alidai upelelezi bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kutajwa.

Hakimu kikoga alisema dhamana kwa washtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, mmoja mfanyakazi kutoka taasisi inayotambulika kisheria, barua za utambulisho na nakala ya vitambulisho vya taifa.

Hata hivyo washtakiwa wote wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi itatajwa tena Oktoba 15 mwaka huu.  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here