23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kizimbani kwa dawa za kulevya

Na GODFREY SHAURI-DAR ES SALAAM

MKAZI wa Bunju A, Dar es Salaam, Hamisi Shabani Mbwana (26), amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa shtaka la kukamatwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Awali, akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Denice Mlashani, Wakili wa Serikali, Violet David alidai Mei 26, mwaka huu, mtuhumiwa alikamatwa na dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa gramu 11.44 eneo la Bunju B.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na upande wa Jamhuri ulisema upelelezi umekamilika na kuomba tarehe ya kusomwa tena kwa shauri hilo.

Hakimu Mlashani alisema kesi hiyo ina dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, wawe wafanyakazi wa Serikali, wawe na vitambulisho vya taifa na barua kutoka Serikali ya mtaa, watakaotoa bondi ya Sh milioni 2.

Mshtakiwa hakukidhi vigezo vya dhamana na alirudishwa rumande.

Upande wa Jamhuri ulisema kesi hiyo itakuja kusomwa tena Septemba 7.

Wakati huo huo, mkazi wa Bunju, Samsoni Eliasi (20) na Mohamed Salum (23), mkazi wa Jangwani, walipandishwa kizimbani kwa tuhuma ya unyang’anyaji kwa kutumia silaha. 

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Hudi Majidi, wakili wa Serikali, Daisy Makalala  alidai kuwa Mei 22, mwaka huu eneo la Bunju, watuhumiwa walimnyang’anya Pasco Buhatwa simu aina ya Infinix yenye thamani ya Sh 260,000.

Watuhumiwa hao pia wanadaiwa kumnyang’anya begi lenye thamani ya Sh 30,000 kisha kumkata na kumsababishia majeraha mwilini.

Washtakiwa walikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ulisema upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe kwa ajili ya kusomwa tena.

Hakimu Hudi alisema kesi hiyo haina dhamana, hivyo washtakiwa watarudishwa rumande hadi Septemba 8.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles