Kizimbani kosa la unyang’anyi kutumia silaha

0
674

Erick Mugisha, Dar es salaam

MKAZI wa kawe Fravian Gasper (35) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kinondoni kwa kosa la Unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Hudi Hudi na Mwendesha Mashtaka wa Jamuhili ASP Hamisi alidai Agosti 4, 2019 eneo la mwenge mataa ya kuongozea magari wilayani kinondoni, Dar es salaam aliiba simu aina ya Huawei yenye thamani ya Tsh 350,000 mali ya John Robert na kabla na baada ulimtishia kwa kisu ilikujipatia mali hiyo.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka hilo mbele ya mahakama na mwendesha mashtaka wa jamuhuri ASP hamisi alidai upeleelzi wa shauri hili hauja kamilika aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa.

Hakimu Hudi alisema kwamuujibu wa sheria na kanuni la kosa hili hautakuwa na dhamana utakuwa ukitokea rumande hadi mwisho wa kesi.

Kesi itakuja kwa kutajwa tena octoba 1 mwaka huu.

Wakati huo huo MKAZI wa Salasala Hassan Martin (24) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kinondoni kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya hakimu Happy Kikoga na Mwendesha mashtaka wa Jamuhili Neema Mushi alidai Octoba 29, 2017 Dar es salaam alikutwa na Laptop aina ya Dell na kebo yake  vyenye thamani ya sh 2,000,000 ikidhaniwa kwamba imepatikana kwa nia ya isiyokuwa ya halali.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka hilo mbele ya mahakama na mwendesha mashtaka wa jamuhili, Mushi alidai upelelezi wa shauri hili  hauja kamilika aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa.

Hakimu kikoga alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa kuwa na wadhamini wawili, moja awe muajiliwa katika taasisi inayotambulika kisheria, barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho vya taifa na kusaini bondi ya sh 1,000,000.  

Mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi itakuja kwa kutajwa tena octoba 10 mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here