24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘Kiwango ugonjwa wa malaria kimepungua’

MWANDISHI WETU

-BAGAMOYO

MRATIBU wa malaria kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Stella Kajange, amesema ugonjwa wa malaria umepungua kwa asilimia 50 ikiwamo kupungua pia kwa maambuzi na vimelea vya ugaonjwa huo kwa asilimia 15 kwa mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.3 kwa mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, mjini Bagamoyo mkoani Pwani,  wakati wa mkutano  wa wadau wa masuala ya malaria, Kajange, alisema kuwa kupungua kwa malaria  kumetokana na mafanikio waliyoyapata kati ya Serikali, wadau na wahisani.

Alisema Tanzania inaendelea vizuri katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria ambao ugonjwa huo umekuwa  ni tishio kwa jamii.

“Licha ya kupungua kwa ugonjwa huu nchini lakini ugonjwa huu bado ni tishio kwa jamii na hivyo serikali inaendelea na utekelezaji wa afua mbalimbali ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua,” alisema Kajange

Aidha aliongeza sera ya mwaka 2007 inaelezea muelekeo wa nchi katika kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na afya njema ili waendelee na shughuli zao mbalimbali za uzalishaji na kujipatia kipato.

 “Serikali ya Tanzania inafanya kazi na wadau mbalimbali wa maendeleo, tunawashukuru sana PMI kwa pamoja na USAID na wadau wengine kwa kutuunga mkono kwa miradi inayotekelezwa sehemu mbalimbali nchini,”alisema Kajange

Naye Msimamizi wa Kitengo cha Kupambana na Malaria Mradi wa Taifa wa kudhibiti Malaria (NMCP),Winfred Mwafongo alisema ugonjwa wa malaria unaathiri zaidi kundi la wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Alisema katika mikakati yao waliyojiwekea ni kuhakikisha wanadhibiti Malaria nchini ambapo tayari wameweka utaratibu wa  afua ambazo zinazohusika na udhibiti wa Malaria.

Alisema miongoni mwa afua hizo ni kuhakikisha kuna kuwepo na matumizi ya vyandarua vyenye dawa ,kuangamiza vijidudu  na upuliziwaji wa viuadilifu kudhibiti mbu.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Mradi wa VectorWorks Waziri Nyoni, alisema mradi huo umedumu nchini takribani miaka mitano ambao ulijikita katika usambazaji wa vyandarua vyenye dawa katika mikoa mbalimbali.

 “Mradi umedumu nchini ndani ya miaka mitano na mwaka huu mwezi September ndio mwisho wa mradi huu,tunaamini kwa ushirikiano tulioupata umeweza kuleta tija kwa jamii katika kuhakikisha wananchi wanatumia vyandarua vilivyowekwa dawa,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles