24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

KIWANDA KIKUBWA CHA DAWA KUJENGWA NCHINI

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kiwanda kikubwa cha kutengeneza dawa kinatarajiwa kujengwa nchini ili kupunguza adha na gharama zinazoikumba nchi wakati wa  kuagiza dawa nje ya Tanzania.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kujadili uwekezaji wa kiwanda cha dawa hapa nchini leo jijini Dar es salaam.

“Leo tumekutana kujadili jinsi ya kuwekeza na kiwanda cha kutengeneza dawa cha FOSUN PHARMA kutoka nchini ili kupunguza changamoto za kuagiza dawa nje ya nchi na kutokomeza tatizo la upatikanaji wa dawa nchini.

“Kiwanda hicho kitapunguza asilimia kubwa ya fedha inayokwenda nje kwa ajili ya manunuzi ya dawa kwani hadi sasa asilimia 94 ya fedha zinakwenda kununua dawa nje na asilimia sita ndiyo inannua dawa nchini,” amsema.

Aidha, Waziri Ummy amesema kutokana na uwekezaji huo itasaidia kupunguza muda wa kuagiza dawa kwani muda mwingine kunachukua miezi tisa hadi miezi 11 kupata dawa kutoka nje ya nchi hivyo kuifanya Serikali kuagiza mzigo mkubwa zaidi ili kukimbizana na mahitaji ya Watanzania.

“Tunatumia muda mrefu sana kupata dawa tangu tunapoagiza na wakati mwingine tunaweza kupata dawa zisizo na ubora kutokana na dawa hizo zinakaguliwa na mdhibiti wa nje hivyo zinaweza zikaruhusiwa tu na zikija kukaguliwa na mdhibiti wa ndani unaweza kukuta hazina ubora,” amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema hakuna kikwazo kwa kampuni hiyo kuanzisha ujenzi wa kiwanda cha dawa hapa nchini kwani kitasaidia upatikanaji wa dawa kwa urahisi na kukua kwa uchumi kupitia viwanda.

“Tumejadili na kuwakubalia bila ya kuweka kikwazo kwani tumeridhishwa na ubora wao katika utengenezaji wa dawa na mafuta nchini kwao hivyo tunawakaribisha kuja kufanya uwekezaji huo,” amesema Waziri Mwijage.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles