28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

KIWANDA CHA KONYAGI CHAENDELEA KUZALISHA VIROBA

 

Na ASHA BANI    

DAR ES SALAAM

LICHA ya kupigwa marufuku kwa pombe za kwenye vifungashio vya mifuko ya plastiki maarufu viroba, kiwanda cha kuzalisha na kusambaza bidhaa za Konyagi, Tanzania Distilleries kilichopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam kimeendelea kuzalisha pombe hiyo ambapo imekutwa shehena kubwa ya pombe hiyo katika ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba, kiwandani hapo leo.

Katika ukaguzi huo wa kubaini wazalishaji,wasambazaji na wauzaji wa kilevi aina ya viroba ili kuweza kuwachukulia hatua za kisheria Waziri Makamba na timu ya watu kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Jeshi la Polisi na Baraza la Mazingira (NEMC), walikuta shehena yenye katoni zaidi ya 100,000 ya viroba vya konyagi na valuers vilivyoonyesha kuendelea kuzalishwa hadi jana ikiwa ni siku ya mwisho ya tangazo la katazo la kuzalisha pombe hiyo.

Aidha, sehemu ya mitambo zilipokutwa pombe hizo zilionyesha mtambo huo umezimwa ghafla huku pombe ikimwagika sakafuni, hata hivyo uongozi wa kiwanda hicho walikuwa wanalazimisha kuwasha CCTV ili kuwaonyesha mitambo hiyo ilizimwa lini.

Baada ya mvutano mkali, Meneja wa kiwanda hicho Davis Deogratius, aligoma kusaini fomu ya idadi ya mzigo aliokutwa nao hadi alipolazimishwa na hatimaye kukubali ambapo, alilalamikia hatua hiyo huku akieleza hasara watakayoipata kutokana na kutouza mzigo huo mkubwa ambao wameuzalisha hadi  Februari 28, kwamba hasara haitapatikana kwa upande wao pekee kwani wameajiri watu wengi hivyo kuna madhara ya wao kuyumba kibiashara.

“Bado tunahangaika na kubadilisha teknolojia hii si jambo rahisi kama inavyofikiriwa kwa sasa tunafanya utaratibu huo,’’alisema Davis.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles