30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Kiwanda cha Axel Chemical chabainika kuwa kwenye makazi

Mwandishi Wetu -Bagamoyo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Zungu, katika ziara ya kushtukiza  amejiridhisha yeye na ujumbe wake kwamba Kiwanda cha Axel Chemical kimejengwa katika makazi ya watu eneo la Zinga wilayani Bagamoyo.

Kiwanda hicho kimebainika kuwa kinatengeneza bidhaa na kuzifungasha kwa jina tofuati na lile ambalo limesajiliwa serikalini.

Akizungumza jana, mmiliki wa kiwanda hicho, Prashant Detha, alikiri makosa aliyoelezwa na Waziri Zungu na hasa kosa la kufungasha bidhaa katika mifuko yenye jina tofauti na lile lililomo katika nyaraka za usajili serikalini.

“Makosa yote tutayarekebisha,” alisikika Detha akimuahidi Zungu alipokuwa akizungumza naye kwa njia ya simu akiwa njiani kutokea nchini India.

Kutokana na hali hiyo Zungu aliagiza kiwanda kifungwe hadi uchunguzi wa kina utakapokamilika kuhusu tuhuma dhidi ya uongozi wa kiwanda hicho, uhalali wake, ulipaji kodi  na Serikali  kujiridhisha kwamba  mapato yake stahiki yamepatikana.

Alisema kitendo cha  kampuni hiyo kuzifungasha bidhaa katika mifuko yenye jina tofauti na nyaraka zilizosajiliwa kimekuwa kikiikosesha Serikali mapato halali.

“Serikali imekuwa ikipoteza mapato kutokana na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara nchini.  Jambo hili  linarudisha nyuma maendeleo,” alisema Zungu.

Alisisitiza kwamba ni lazima uchunguzi ufanywe ili kubaini tuhuma zilizopo ikiwa ni pamoja na kulituhumu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwa linachelewesha ajenda ya uwekezaji, jambo ambalo si la kweli.

“Kazi kubwa inayofanywa na NEMC ni kuhakikisha uwekezaji unafanyika kama azma ya Serikali inavyotaka; lakini uwekezaji ufanywe kwa kufuata sheria na kanuni ili kulinda mazingira,” alisema Zungu.

Alisema ujumbe wake umebaini mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kiwanda kufanya shughuli za uzalishaji kwa muda mrefu bila cheti cha tathmini ya athari kwa mazingira,  jambo ambalo amesema ni kinyume cha utaratibu na kwamba kiwanda hakitambuliki wilayani japo kimekuwa kikifanya kazi toka 2014.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,951FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles