25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Kituo kingine cha redio chapigwa faini ya Sh mil 9/-

Na BRIGHITER MASAKI -DAR ES SALAAM.

MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imekipiga faini ya shilingi milioni 9 kituo cha redio cha Passion Fm kwa kurusha maudhui pasipo kuwepo kwa mizani ya habari jambo  ambalo ni kosa kisheria.

Kituo hicho pia kimetakiwa kuomba radhi kwa muda wa siku tatu kuanzia Novemba 14 hadi 16 mwaka huu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati ya maudhui TCRA, Valeli Msoka, alisema kamati ilibaini kituo hicho kilirusha maudhui yasiyokuwa na mizani jambo ambalo ni uvunjifu wa sheria.

“Watangazaji wanatakiwa kuzingatia mizani ya habari kabla ya kutangaza maudhui, kituo hicho tumebaini kuna tatizo la watendaji kutokana na kukosa vigezo vya kuwa watangazaji”alisema

Alisema kamati ya TCRA ilipokea malalamiko kutoka kwa Khadija Palamana juu ya kulalamikia kituo hicho kwa kumchafua kufuatia kutoa habari pasipo kumuhoji.

“Baada ya kupokea malalamiko hayo na kuwaita wote kwa pamaja na kuwasikiliza TCRA inataka kituo hicho kumuomba radhi.

“Wanatakiwa kumwomba radhi Khadija kwa muda wa siku tatu, mara tatu kwa siku kuanzia Novemba 14 Novemba 16 na kupitia kipindi chao cha Jogoo la shamba”alisema

Aidha kamati hiyo ilikishauri chombo hicho cha habari kuwa na watangazaji wenye sifa ili kufuata sheria za utangazaji.

“Hii imeonyesha kuwa chombo hicho kina watangazaji wasio na sifa wasiofata weledi na sheria za utangazaji.”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles