23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kituo kidogo cha damu salama Kasulu kusaidia kupungua za vifo…

Na Editha Karlo,Kasulu

Ujenzi wa kituo kidogo cha kuhifadhi damu salama wilayani Kasulu mkoani Kigoma kilichojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Msalaba Mwekundu(Redcross) kinaelezwa kuwa kitachangia kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua.

Katibu Tawala wa Mkoa Kigoma, Rashidi Mchatta akizungumza na www.mtanzania.co.tz leo Mei 7, 2021 wakati wa uzinduzi wa kituo hicho amesema kuwa kwa sasa mkoa Kigoma unakuwa na vituo viwili vidogo vya kuhifadhi damu hivyo kuwa rahisi na uhakika wa upatikanaji wa damu kwa haraka.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Rashid Mchatta akikata utepe kwaajili ya kuzindua kituo kidogo cha damu salamu katika Hospital ya Wilaya ya Kasulu kilichojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Msalaba Mwekundi(Redcross).

Mchatta amesema kuwa mkoa Kigoma una vituo vya afya 34 vinavyofanya upasuaji wa dharula ambavyo wakati wa upasuaji huo kiasi kikubwa cha damu kinahitaji hivyo mara nyingi uhalazimika damu kutolewa hospitali ya mkoa Kigoma Maweni au Tabora jambo ambalo limekuwa likichangiwa kupoteza maisha ya wagonjwa.

“Kwa sasa kituo hicho kitasaidi kuhudumia wilaya za Kakonko, Kibondo,Buhigwe, sehemu ya wilaya Uvinza na wilaya ya Kasulu na hivyo uwepo wake na muhimu kwa afya za wananchi wa mkoa Kigoma,” amesema Mchatta.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Felician Mtahengerwa amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho umewezeshwa kwa ufadhili wa Shirika la Msalaba mwekundu la Hispania kupitia mifuko yake ya wahisani mbalimbali waliopo nchini humo.

Mtahengerwa amesema kuwa kwa sehemu kubwa fedha hizo ni michango ya wananchi wa Hispani ambao wanachangia watu wenye shida maeneo mbalimbali duniani na kwamba kufanya kazi yenye tija kunatoa motisha kwa wafadhili kuongeza misaada yao akitaka pia watanzania kuiga mfano huo kwa kujitolea kwa wingi kuchangia mifuko ya hisani ili iweze kusaidia utekelezaji wa miradi ya wananchi.

Mratibu wa mpango wa damu salama mkoa Kigoma kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania, Habichi Maramba amesema kuwa kiasi cha Sh milioni 85 kimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha damu salama.

Maramba alisema kuwa ujenzi huo umezingatia mahitaji ya uwepo wa kituo cha kuhifadhia damu hasa wakati idadi kubwa ya watu wanapojitolea damu hivyo damu hivyo hulazimika kupelekwa kituo kidogo cha Hospitali ya mkoa Kigoma Maweni au Tabora.

Akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Simon Hanange, Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Titus Mguha amesema kuwa uwepo wa kituo ni jambo moja lakini wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi kujitolea damu ili lengo la kituo kuwa na damu ya kutosha wakati wote kwa ajili ya kusaidia wagonjwa liweze kutimia.

Kwa sasa Mkoa Kigoma unahitaji kiasi cha lita 1,870 za damu kwa mwezi lakini ni lita 1,200 pekee zinazokusanywa kwa mwezi jambo ambalo jitihada za ziada zinahitajika kuhakikisha damu ya kutosha inakusanywa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles