24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Kituo cha tiba kwa Waviu chafunguliwa Mirerani

Na MOHAMED HAMAD -SIMANJIRO

KUFUNGULIWA kituo cha tiba na matunzo (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (WAVIU) katika mji wa Mirerani wilayani hapa, kutapunguza asilimia 16 ya maambukizo ambayo yanazidi kitaifa.

Akifungua kituo hicho, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Watu wenye Ulemavu, Jenister Mhagama, alisema mafanikio hayo yanatokana na jitihada za Rais Dk. John Magufuli kutaka wananchi waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na Serikali yao.

Alisema kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya afya, elimu na miundombinu ambayo wananchi wanaendelea kuyashuhudia katika maeneo yao.

 “Jambo hili tunaweza kuliandika katika orodha ya mambo ambayo yametekelezwa na Rais Magufuli ambalo ni la kiilani, lakini pia la kikatiba, kuboresha huduma za afya kama haki ya wananchi wa Wilaya ya Simanjiro na Mirerani,” alisema.

Alisema Sheria ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Na. 22 ya mwaka 2001 inaelekeza kulinda haki za watu wanaoishi na VVU Ukimwi (Waviu), kutoa huduma bora na kuondoa ubaguzi na NA. 28 ya mwaka 2008 na Sera ya Taifa ya Ukimwi ya mwaka 2001 zinatoa wajibu wa kila mtu kilinda na kutetea haki za Waviu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Masuala ya Ukimwi, Oscar Rwegasira Mukasa, alisema Serikali imejipanga kutunisha Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) kupitia wadau wengine ambao utachukua nafasi kubwa kama suluhisho la mapambano dhidi ya Ukimwi.

“Mpaka leo tunavyoongea asilimia  95 ya fedha zote za mapambano ya Ukimwi zinatoka nje ya nchi, jambo ambalo linaonyesha hatujaanza kujitegemea vya kutosha, hata hizi jitihada zinazoonekana leo ni kutokana na mchango mdogo huo wa ATF, tukiuboresha zaidi tutakuwa na mafanikio makubwa,” alisema. 

Mwenyekiti wa Bodi ya ATF, Godfrey Simbeye, alisema toka mfuko huo uzinduliwe umekusanya Sh bil 2.7 na matunda yake ni ujenzi wa vituo kikiwemo CTC Mirerani.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Manyeti alisema maambukizi ya Ukimwi mkoani mwake siyo makubwa.

“Tathmini ya sasa maambukizo ya Ukimwi Manyara ni asilimia  2.3 kitaifa, Wilaya ya Simanjiro ni asilimia 1.9, kwa mji wa Mirerani ni asilimia 16, tafsiri yake ukilinganisha na Mkoa wa Kilimanjaro, Manyara iko chini kwa maambukio,” alisema.

Alisema Serikali lazima ichukue tahadhari, kwani watu wa Mirerani wanaangamia na maambukizo yanaongezeka kila kukicha.

 “Ukimwi umekalia pabaya, unahitaji kukumbushana kwa kuombana na kuambizana taratibu bila jirani kusikia. Ungekuwa unahitaji jeshi kama lile linalolinda ukuta, ningeleta mara moja,” alisema.

Mbunge wa Simanjiro, Jemes ole Milya (CCM) alipongeza jitihada za Serikali akidai hakuna mwananchi asiyefahamu kinachofanyika hivyo inawarahisishia kazi kuongoza wananchi.

Naye Mbunge Viti Maalumu Martha Umbula (CCM), alisema kituo cha tiba na matunzo kwa WAVIU (CTC) kitasaidia wananchi kutambua afya zao.

Bodi ya ATF kupitia TACAIDS imetoa msaada wa Sh mil 250 ambapo Sh mil 200 ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo na Sh mil 50 ununuzi samani na vifaa tiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles