27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kituo cha kulelea watoto yatima Isoko chaelemewa

Na Denis Sikonde, Songwe

Ukosefu wa kipato cha kutosha umesababisha kituo cha kulelea watoto yatima cha Isoko(ISOKO HOSPITAL OPHANS PROJECT) wilayani Ileje mkoani Songwe kupunguza idadi ya watoto kutoka 1,887 mwaka 2018 hadi 238 mwaka 2022.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha kituo hicho, Enea Asangalwisye Kajange wakati ya siku ya kumbukuzi ya kuadhimishwa kuanzishwa Kwa kituo hicho mwaka 1996 huku wanafunzi 105 wa msingi na sekondari wakipewa mahitaji ikiwamo mbuzi na cherehani.

Kajange amesema kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kutoa msaada kwa watoto hai ikiwepo daftari, masweta, mbuzi, cherehani ambapo vifaa hivyo wamekabidhiwa walezi watakaosaidia kuvitunza vifaa hivyo.

“Katika kumbukizi ya siku hiyo tumefanikiwa kukabidhi mbuzi 100 Kwa watoto 100 wenye thamani ya Sh 800,000 ambapo Kila mtoto amepewa mbuzi 1, cherehani Kwa wanafunzi wa chuo cha Ufundi kituoni hapo, masweta, daftari na biki Kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu Kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari,” amesema Kajange.

Kajange amesema kituo hicho kinalea watoto kutoka kata 3 za Kafule, Ikinga na Ngulugulu ambapo awali kata zote 18 zilifikiwa na kituo hicho lakini kutokana na kutojitosheleza kifedha kata 15 zimeondolewa.

Aidha, Mkurugenzi huyo amesema kutohudumia watoto wilaya nzima kumetokana na uhaba wa kifedha kwani watoto wengi wanahitaji msaada hivyo kuomba maahirika kusaidiana na kituo hicho ili kusaidia taifa la kesho.

Laisoni Kalinga ni mmoja wa walezi wa watoto hao amesema kituo hicho kimekuwa ni msaada kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu Kwa kuwapa msaada wa mahitaji muhimu ikiwepo vifaa vya shule hali inayopelekea watoto kuishi katika mazingira rafiki.

‘Watoto hawa tumekuwa tukiwalea kwa msaada wa kituo cha Isoko Ophans Project kwa kupewa mahitaji ya shule, lengo ni kuwafanya waishi kama watoto wengine hivyo tunaahidi kutumia nafasi hii kushirikiana na Mkurugenzi Enea Kajange kadili mungu atakapomjalia uzima nakuwasihi wadau kuunga juhudi Kwa watoto wengine wilayani humo,” amesema Kalinga.

Akizungumza kwaniaba ya watoto yatima kituoni hapo ,Semeni Mshani amesema kituo hicho kimekuwa ni mkombozi Kwa watoto waliopoteza wazazi wao kwani hupataahitaji kama wengine, kama yeye anavyonufaika Kwa kusoma chuo cha ufundi faninya cherehani na kunufaika na msaada wa kupewa cherehani.

Ikumbukwe kuwa Julai kila mwaka kituo hicho huadhimisha kuanzishwa kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima kama faraja ya kuwajenga kiimani na kisaikolojia Ili waendelee kuishi kama watoto wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles