25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

KITILA AIPA MTIHANI DAWASCO

Na Frank Shija – MAELEZO


KAMPUNI ya Usambazaji Maji Dar es Salaam na Pwani (DAWASCO) na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), zimetakiwa kuongeza kasi ya usambazaji maji, ili kufikia malengo ya Serikali katika kuwatumikia wananchi kwa kuwapa huduma za msingi.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo, wakati akizungumza na menejimenti ya mamlaka hizo.

Alisema licha ya ongezeko la upatikanaji wa maji, ipo changamoto ya idadi kubwa ya wananchi kutofikiwa na huduma , hivyo ni lazima mamlaka husika kuongeza kasi ya usambazaji wa miundombinu ya maji katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa.

“Pamoja na kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha upatikanaji wa maji hakikisheni mnaongeza kasi ya usambazaji wa huduma hii muhimu kwa wananchi, kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatendea haki dhana ya kuwa mnaongoza kwa mapato lakini pia mnatoa huduma stahiki kwa wananchi,” alisema Profesa Kitila.

Aidha Profesa Kitila alitoa rai kwa wateja wote wa Dawasco na Dawasa zikiwemo taasisi za umma kutii agizo la Rais Dk. John Magufuli kwa kulipia huduma wanazopatiwa ili kuwezesha mamlaka hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Usambazaji wa Maji Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja, alisema uzalishaji maji umeongezeka  kutoka lita za ujazo milioni 160 kwa siku hadi kufikia lita milioni 271 kwa siku ambazo ni sawa na asilimia 100.37  ya lengo la upatikanaji wa maji.

Katika kuhakikisha inafikia azma ya kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma ya maji kwa wananchi Dawasco inaendesha kampeni ijulikanayo  kama “Mama Tua Ndoo ya Maji Kichwani Ndani ya Siku 90”.

Kampeni hiyo inalengo la kuwaunganisha na huduma ya maji wateja takribani 151,000 katika eneo linalopakana na Barabara ya Morogoro. Kampeni hiyo imeanza Aprili mosi, mwaka huu na ukomo wake utakua Juni 30, 2017.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles