28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kitengo cha Dharura Muhimbili kimefanikiwa kupunguza vifo kwa asilimia 40

Amina Omari, Tanga

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema uwepo wa kitengo cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) umesaidia kuokoa vifo kwa zaidi ya asilimia 40.

Ameyasema hayo leo Ijumaa agosti 2, wakati akizindua jingo la huduma ya dharura na wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo iliyoko mkoani Tanga.

“Kuimarika kwa huduma hiyo kumesaidia kuokoa wagonjwa wengi ambao awali walikuwa wakipoteza maisha kutokana na ukosefu wa huduma hiyo,” amesema.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Leonard Subi amesema serikali imejipanga kujenga majengo ya huduma hiyo katika hospitali 28 za Rufaa nchi nzima.

“Licha ya kujenga tutaweka vifaa tiba na wataalamu ambao ni mabingwa wa kuhudumia katika kitengo hicho lengo ni kuhakikisha tunapunguza vifo vinavyoweza kuzuilika kwa kiasi kikubwa,” amesema Dk. Subi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles