Kitale: Sina fedha za kuanzisha kundi la sanaa

kitale_mussaNA ESTHER GEORGE

MSANII wa filamu na vichekesho, Musa Kitale ‘Mkude Simba’, amesema hana mpango wa kuanzisha kundi la vijana wenye vipaji kwa sasa kwa kuwa hana fedha za kumudu shughuli hiyo.

Alisema lengo lake ni kuanzisha kundi lakini kwa sasa hayupo tayari kwa kuwa hana fedha za kutosha.

“Kwa kweli mpango wa kuwa na vijana ninao, kuna vijana wengi wenye vipaji na wanahitaji kufikia malengo kama yangu, kikubwa ni kwamba sina uwezo wa kifedha lakini mambo yakiwa mazuri nitaweza kufanya hivyo,” alieleza Kitale.

Aliongeza kwamba jambo hilo ni jema na lina malengo mazuri ya kufikisha elimu hiyo kwa wengi lakini kwa sasa sina fedha ila lipo katika mipango yangu ya baadaye.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here