30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Chuo cha SAUTI chakabidhiwa kitabu cha historia ya kisiwa cha Ukerewe

Na Sheila Katikula,Mwanza

Malikale na kitabu cha historia ya asili ya kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza kilichoandikwa mwaka 1895 na Mtanzania wa Kwanza kutoka wilayani Ukerewe, Anicet Kitekeza vimekabidhiwa katika Chuo cha Mtakatifu Agustine (SAUTI) kilichopo jijini Mwanza.

Akizungumza Julai 27, jijini Mwanza mara baada ya kukabidhi malikale na kitabu hicho Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Colorado Denver kilichopo nchini Marekani Profesa, Charles Musiba amesema vitu hivyo vilikuwa vimehifadhiwa tangu mwaka 1968 kwenye chuo kikuu cha St. Olaf University Minnesota Marekani.

Prof. Musiba amesema malikale hizo zitahifadhiwa kwenye Chuo Kikuu cha Sauti ili kutoa elimu kwa wahitimu mbalimbali na watafiti ili waweze kuelewa historia ya ukerewe na tamaduni zao.

Naye Makamu Mkuu wa SAUTI, Profesa Costa Mahalu amesema licha ya kuhifadhi malikale hizo bado kuna umuhimu wa kutafuta kabuli lake ili kuweka historia itakayowasaidia watafiti kuandika historia yake.

“Malikale zilizorejeshwa katika chuo hiki ni pamoja na jembe la asili ya ukerewe, picha za asili ya mkerewe, shoka, nakala za kitabu kilichoandikwa na Kitereza kwa lugha ya Kikerewe chenye jina “Bwana Nyombekele na Bibi Bugonoka Ntulanalwo na Bulihwali, wamekabidhi barua za Kiingereza alizokuwa anamwandikia rafiki yake mzaliwa wa Marekani, Gerald Hartwig ambaye ni mtafiti katika Sayansi ya Utamaduni (Anthropology).

“Mali kale hizi tutazitumia kuhamasisha wageni kutembelea kwenye chuo chetu cha SAUT kwa ajili ya kujifunza utamaduni wa kabila la Wakerewe na zitarahisisha wanafunzi wanaofanya utafiti kuhusu kabila la Wakerewe kupata taarifa,” amesema Prof Mahalu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles