Kiswahili chapendekezwa kutumika Ukanda wa Maziwa Makuu

0
680

Mwandishi Wetu, Brazzaville

Tanzania imeziomba nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu kuridhia kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi na lugha ya kazi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro ametoa ombi hilo jana katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa ukanda wa maziwa makuu, uliofanyika mjini Brazzaville.

“Tumewaomba wenzetu wa maziwa makuu wakubali lugha ya Kiswahili kutumika kama lugha rasmi na lugha ya kazi katika nchi zote za maziwa makuu.

“Pia nchi sita ambazo zipo hapa na hazijaridhia mabadiliko ya mkataba wa Afrika kuruhusu Kiswahili kutumika kama lugha rasmi katika Afrika (AU) nchi hizo zimetuhakikishia kuwa zitaridhia mabadiliko hayo ili kuhakikisha kuwa Kiswahili kinaanza kutumika kama lugha rasmi ya kazi,” amesema Dk. Ndumbaro.

Dk. Ndumbaro amesema matumizi ya lugha ya Kiswahili katika ukanda huo ni fursa ambayo italeta umoja wa kitaifa na katika ukanda wa maziwa makuu lakini pia umuhimu wa Kiswahili kwamba ni lugha pekee ambayo haina uhusiano na ukoloni barani Afrika.

Nchi sita ambazo hazijaridhia mabadiliko ya mkataba wa Afrika kuhakikisha kuwa Kiswahili kinatumika kama lugha rasmi ya kazi ni pamoja na Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan, Uganda na Zambia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here