23.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 20, 2021

Kisiwa cha Tefu walilia kivuko, temesa yawajibu

Benjamin Masese -Ilemela    

SIKU chache  baada ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kupokea  kivuko cha MV. Ilemela na kuanza kusafirisha abiria kutoka Kayenze hadi Kisiwa cha Bezi mkoani Mwanza, baadhi ya wakazi wa visiwa vingine  wameomba Mbunge  wa Jimbo la Ilemela, Dk. Angeline Mabula kuishauri serikali ili iweze kuweka ratiba ya usafiri huo  na ifike katika visiwa vingine.

Maombi hayo ya wananchi yalitolewa jana wakati wakizungumza na waandishi baada ya kivuko hicho kuanza  kazi  ya kuwasafirisha abiria kutoka Kayenze hadi Kisiwa cha Bezi kwa Sh 1,000 huku wale wanaoishi Kisiwa cha Tefu, wakiomba  kusaidiwa usafiri huo.

Mkazi wa Tefu, Salome Isack alisema anaomba usafiri wa kivuko hicho cha MV Ilemela kiweze kufika hadi katika kisiwa chao kwani  wamekuwa wakikabiliawa na changamoto ya usafiri.

Naye Afuadi Issa mkazi wa Kayenze alipongeza uwepo wa Kivuko cha MV Ilemela na kusema kwamba  usafiri huo  utakuwa wa kudumu na  utawasaidia kusafiri kwa usalama zaidi tofauti na ilivyokuwa kwa usafiri wa mitubwi na boti.

Kutokana na kilio hichocha wananchi, MTANZANIA ilimtafuta Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),  Mhandisi Japhet Masele ili kutoa ufafanuzi  kuhusu maombi hayo ya wananchi, alisema kivuko cha MV Ilemela hakitaweza kwenda Kisiwa cha Tefu kwa sababu kuna mawe makubwa ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa kivuko na abiria.

Alisema baada ya Kivuko cha MV Ilemela kuanza kazi ya kubeba abiria wa Bezi na Kayenze, wamekubaliana na wamiliki wa boti na mitumbwi iliyokuwa ikifanya kazi Kayenze na Bezi itaelekezwa Tefu na maeneo mengine.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,961FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles