30.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kisa cha mwanamke aliyepoteza mtoto kwa uzembe wa manesi

Na AVELINE KITOMARY

“SITASAHAU siku ambayo nilijifungua mtoto wangu wa kwanza katika hospitali moja hapa jijini Dar es Salaam. Baada ya kujifungua mtoto yule, wahudumu walinitelekeza wakaniacha nisijue la kufanya.

“Kwa sababu ya uchovu wa kujifungua, nilijikuta napitiwa na usingizi, ilipofika saa tisa usiku nilishtuka kutoka usingizini na kuona mtoto wangu akiwa amezidiwa na kubadilika rangi na kuwa wa kijani, niliogopa mno.

“Nilivyoona hivyo nikatoka haraka huku nikikimbia kuelekea kule walikokuwa manesi, nilipofika niliwakuta wakiwa wamelala, nikawaamsha na kuwaambia wakamuone mtoto wangu amebadi lika rangi,” hii ni kauli ya Clara Mboya, mama aliyekumbwa na madhila wakati wa kujifungua mtoto wake wa kwanza.

Licha ya kuwa mama wa watoto wa tatu sasa, uzazi wa mtoto wake wa kwan- za umemuachia kumbukumbu isiyofutia akilini mwake kutokana na changamoto alizokutana nazo wakati wa kujifungua. Clara anasimulia namna alivyoshikwa uchungu wa mtoto wake huyo wa kwanza na kufikishwa hospitalini (hakutaja jina la hospitali), lakini alivyofika na kupimwa akaambiwa njia ya uzazi bado haijafunguka.

Jambo la kushangaza ni kwamba, licha ya kutoka mbali hadi kuifikia hospitali hiyo, alipofika hakupata ushirikiano wowote kutoka kwa muuguzi wa zamu, ambaye kwa makusudi hakutaka kumpa kitanda ili apumzike, badala yake alim- wambia arudi nyumbani.

Anasema muuguzi huyo alimwambia kuwa njia yake haijafunguka hivyo anatakiwa kurudi nyumbani na arudishwe kesho yake.

Anabainisha kuwa kwa kauli hiyo ya nesi walijikuta hawana namna yoyote zaidi ya kurudi nyumbani licha ya kwamba muda ulikuwa umekwenda ili kuwa ni majira ya saa kumi jioni.

“Niliendelea kuumwa tumbo na mgongo, usiku mzima nilikosa usingizi huku nikijisikia vibaya, nilivumilia maumivu hayo hadi kulipokucha tukaanza safari ya kurudi tena hospitalini.

“Tulivyofika nikamkuta yule yule nesi ambaye nilikutana naye jana yake

akanirudisha nyumbani, nikamwambia bado naumwa tangu jana, akanipima tena akasema bado njia haijafunguka.

“Yule mama niliyeambatana naye kwenda hospitalini akamwambia yule nesi kwamba sasa hivi harudi nyumbani, tunaomba kitanda apumzike na kama ni mazoezi basi niendelee kuyafanya nikiwa hapo,” anaeleza Clara.

Hata hivyo, anasema baadaye alipata kitanda huku akiendelea kufanya mazoezi hadi ilivyofika saa kumi ambapo uchungu ulianza kuchanganya na ku- pelekwa sehemu ya kujifungulia (leba).

“Nilivyofika leba bado sikupatiwa hu- duma nzuri, nilikuwa nikiwaita manesi hawaji hasa ukizingatia kuwa walikuwa wawili tu, yaani ilikuwa unaita hadi unachoka hawaji mwishowe nikanyamaza.

“Nilikuwa najisikia kujifungua lakini ukimwita nesi haji, mwishowe niliishiwa nguvu, kwa bahati nzuri akaja nesi mmoja ambaye ni mwanamume, alikuwa amemaliza zamu yake lakini sikusita kumnweleza shida yangu.

“Nilimuita akaniuliza shida yangu nikamwambia naumwa hadi nahisi kuishiwa nguvu,” anasimulia Clara.

Anasema baada ya yule nesi kuonekana kumsikiliza, ilimlazimu kumuahidi fedha mara atakapomsaidia kujifungua salama.

Anasema hata hivyo, nesi huyo alikataa ofa hiyo akiahidi kumsaidia bila malipo licha ya kwamba muda wake wa kazi ulikuwa umekwisha.

“Namshukuru alinisaidia kwa kiasi kikubwa hadi nikafanikiwa kujifungua salama. Alikuwa akiniminya tumbo
kwa sababu nilishaishiwa nguvu kabisa, sikuweza kufanya chochote bila msaada wake.

“Mtoto aalipotoka akaniambia yupo vizuri na alilia kama ambavyoinatakiwa, kwa kifupi hakuwa na shida yoyote.

“Aliponikabidhi mtoto wangu aliniambia nipumzike hadi kesho yake asubuhi nitakapopata ruhusa ya kurudi nyumbani,” anaelezea Clara.

Clara anasema changamoto hazi

kuishia hapo kwani baada ya mtoto kuzaliwa maziwa yalikuwa hayatoki hali iliyosababisha mtoto alie mara kwa mara.

“Mtoto alikuwa analia muda wote, nawaita manesi na kuwaambia kuwa mwanangu analia na huu ni uzazi wangu wa kwanza, maziwa hayatoki sijui la kufanya lakini hawakujali.

“Nilijaribu kuomba nisaidiwe maziwa hata ya kopo ili nimpe mtoto anyamaze lakini sikupata msaada wowote, badala yake waliniambia kuwa anaweza kukaa hadi kesho asubuhi bila kula chochote na asipate shida.

“Kwa kuwa sikuwa nafahamu cho- chote, niliwasikiliza na kuona kawaida, nilijaribu kuminya maziwa kama yata- toka lakini sikufanikiwa, nikaacha.

Anasema baada ya mtoto kulia kwa muda muda mrefu, ndipo akabadilika, aliwaita manesi na kuwaeleza ndipo wakaanza kuangalia mafaili na kadi yake.

“Baada ya hapo wakaniambia niwasubiri watakuja, nilikaa kitandani kuwasubiri huku natetemeka, mara wakaja kumchukua.

“Asubuhi akaja nesi mwingine tofauti na wale wa usiku. Aliniuliza unajisikiaje nikamwambia nimeishiwa nguvu natetemeka, akaniambia kwani umetoka damu nyingi nikamwam-
bia sijui, akaniambia sawa nyanyuka twende ukamwone mtoto wako.

“Nilipofika nilimkuta amewekewa dripu na wakaniambia kuwa wamemchoma sindano hivyo natakiwa kulipia.

“Niliwaambia kwamba kwa wakati ule sikuwa na fedha, maana hata begi langu nilikuwa silioni kwahiyo hela italipwa kesho na baba yake atakapokuja, akasema Sawa,” anasimulia Clara.

Anaeleza kuwa alivyorudi kitandani akawa anatafakari sababu za mtoto wake kuugua na kubadilika rangi.

“Ni kwanini wamenipa huduma mbaya? Ukizingatia kuwa ilikuwa ni hospitali binafsi, nililipia fedha nyingi si kwamba nilikuwa natibiwa bure,

maswali haya yote yalikosa majibu,” anahoji.

“Baadae nilitakiwa kwenda kum- nyonyesha mwanangu, lakini nilipofika sikumkuta yule mhudumu wa awali, niliposimama mlangoni kumsubiri aka- ja, akaniuliza wewe ni nani nikamtajia jina langu na la mtoto wangu akasema kanisubiri nitakuja kukuita.

“Nilimsubiri lakini hakuja, baadae akaja nesi mwingine akaniuliza wewe ndio fulani, nikamwambia ndio mimi, akaniambia nieleze jinsi ulivyofika hadi kujifungua… nikamweleza,” anasema.

Anasimulia kuwa baada ya
nesi huyo kupata maelezo yake akamuuliza.”Nani wamekuja hadi sasa, nikamwambia mume wangu amekuja yuko nje, akaniambia nikamwite ili twende ambako mtoto alikuwa ame- pelekwa.

“Tulivyofika nikaambiwa mtoto wangu amefariki, nililia kwa uchungu, mume wangu alikuwa amekuja na bahasha aliitupa pale pale akaondoka zake,” anaeleza huku akifuta machozi.

WANAWAKE WANATAKA NINI?

Clara anasema suala la uzazi linahi- taji huduma nzuri na wahudumu kuwa karibu na wazazi.

Kwa wanawake wengine hili limedhihirika baada ya Muungano wa Utepe Mweupe na Uzazi Salama Tanzania (White Ribbon), kufanya kampeni katika maeneo mbalimbali nchini.

Kampeni hizo zilizofanyika katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Lindi, Mara, Mt- wara, Mwanza, Shinyanga na Tabora, ilihusisha wanawake na wasichana 110,000 kutoka mikoa hiyo.

Kwa mujibu wa Mratibu wa utepe huo, Rosemary Mlaya, katika kampeni hizo wanawake hao waliainisha map- endekezo 10 waliyotaka yawepo katika huduma za uzazi.

Anasema asilimia 8.99 ya wanawake walipendekeza upatikanaji wa damu

salama inayotolewa bure, kuongezwa kwa vifaa na vitendea kazi vya kujifun- gulia.

“Asilimia 8.61 wanahitaji huduma za uzazi zenye heshima na utu ambazo pia ni rafiki na watoa huduma wenye adabu. Asilimia 7.56 walihitaji huduma zilizoboreshwa, ustawi na afya ya uzazi.

“Asilimia 7.32 walihitaji kuongezwa kwa vituo vya afya, vinavyofanya kazi kwa ukamilifu na viwe karibu na kina mama na wasichana huku asilimia 7.17 wakihitaji ushauri nasaha na ufahamu kuhusu afya ya uzazi.

Mlaya anasema kitu kingine amba- cho walikuwa wanakihitaji, asilimia 7.03 ya wanawake ni taarifa kuhusu uchungu na kujifungua na uwapo wa watoa huduma wakati wote.

“Wengine asilimia 5.41 walitaka kuongezwa watoa huduma wenye stadi na mazingira mazuri ya kazi kwa watoa huduma, wengine asilimia 4.41 walihitaji upatikanaji wa maji safi na vyoo safi na asilimia 4.18 walitaka uwapo
wa vitanda, mashuka na magodoro,” anabanisha Mlay.

Anasema Novemba mwaka jana, matokeo ya kampeni hiyo yaliwasilishwa bungeni ambapo jumla ya wabunge 60 wanaounda kikundi cha wabunge wabobezi wa masuala ya uzazi salama walishiriki, ikiwa ni pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

TAMKO LA SERIKALI

Katika kipindi cha miaka mitano, serikali imekuwa ikiendelea na ujenzi wa majengo maalum ya mama na mto- to katika hospitali za rufaa ikiwamo Mwananyamala.

Hatua hiyo inalenga kuboresha hu- duma ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Leonard Subi, anasema utafiti mdogo uliofanywa hivi karibuni unaonesha

vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka 1,744 mwaka 2018 hadi kufikia 1,657 kwa mwaka 2019.

Dk. Subi anasema sababu za kupun- gua kwa vifo hivyo ni baada ya serikali kuendelea kuboresha huduma za afya ili kila mtu apate huduma bora hivyo, mwananchi kupata huduma ni haki yake.

“Katika kipindi cha miaka minne, serikali imeweza kujenga hospitali 70 ambapo miaka zaidi ya 50 ya uhuru kulikuwa na hospitali 77.

“Katika kila mkoa mpya tumejenga hospitali na vituo vya afya 540 na vingine kukarabatiwa.

“Tumeboresha Miundombinu ya vi- tuo vya afya 361 lengo letu ni kuwasikiliza wanawake wanachotaka hivyo, idadi ya kina mama wanaojifungulia vituo vya afya imeongezeka, mwanzo ilikuwa asilimia 63 lakini sasa wamefikia asilimia 79,” anabainisha Dk. Subi.

Anasema upatikanaji wa dawa umeongezeka ambapo sasa hivi dawa muhimu zinapatikana kwa asilimia 94 huku chanjo zinapatikana kwa asilimia 98.

“Ongezeko hilo limetokana na kuongezwa kwa bajeti ya dawa kutoka Sh bilioni 30 hadi Sh bilioni 270.

Pia anasema serikali itachukulia kwa uzito vitu ambavyo wanawake wa navitaka ili waweze kufurahia huduma za uzazi ikiwamo mazingira bora.

“Hivyo, vitu ambavyo wanawake wanataka tutavichukua na kuvifanyia kazi, tunataka wanawake wafurahie hu- duma za uzazi kwa sababu ni sehemu muhimu zaidi ya mwanzo wa binada- mu, tutafuatilia mambo yote ikiwamo hilo la kuongeza wahudumu wa afya,” anaeleza Dk. Subi.

Pia anasema kwa kushirikiana
na Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na taasisi zingine za serikali na zisizo za kiserikali wa natarajia kukamilisha utafiti wa vifo vitokanavyo na uzazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles