29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kipingu aibua vipaji lukuki Muheza

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MDAU maarufu wa soka hapa nchini, Kanali mstaafu Iddi Kipingu, amefanikiwa kuibua vipaji lukuki vya soka Muheza, Tanga,  kupitia progamu inayoendelea wilayani humo.

Akizungumza kutoka Muheza, mratibu wa programu hiyo, Michael Maurus, alisema kuwa tangu wameanza wiki mbili zilizopita, wamepokea vijana zaidi ya 150, wakiwani wa kike na wa kiume.

Alisema kuwa programu yao hiyo ya kusaka vipaji vya soka chini ya taasisi ya Kipingu Sports Academy, pia itapiga hodi katika mikoa ya Shinyanga, Kagera na Rukwa.

“Tunashukuru Mungu vijana wamejitokeza kwa wingi katika mpango wetu huu wa kuibua vipaji vyasoka, tukilenga kuzalisha wachezaji ambao watakuwa tegemeo la Taifa kwa siku za usoni.

“Sote tunafahamu kuwa nchi yetu kwa sasa ipo katika joto la soka kutokana na mafanikio ya klabu zetu za Simba na Yanga kimataifa na ushiriki wa timu yetu yaTaifa, Taifa Stars kwenye michuano ya Afcon (Kombe la Mataifaya Afrika) nchini Ivory Coast.

“Pia, tukumbuke tutakuwa wenyeji wa fainali za Afcon 2027, hivyo michuano hiyo inatakiwa kutukuta tukiwa na hadhina ya wachezaji wa kila rika kwani ni jukwaa tosha la kunadi vipaji na soka letu kwa ujumla,” alisema Maurus.

Alisema kwasasa Kanali Kipingu anayesifika kwa kuibua vipaji lukuki vya soka vilivyotamba nchini, yupo jijini Dar es Salaam kuandaa mazingira ya kuwanadi wachezaji waliowaibua Muheza.

Maurus aliwashukuru wadau kadhaa kwa sapoti na ushirikiano ambao wamekuwa wakiwapa, hao wakiwa ni Ofisa Utamaduni wa wilaya hiyo, Msafiri Nyaluva na madiwani Hamis Mkodingo (Kicheba), Papaa Bahari (Potwe) pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Muheza, Yusuph Majisafi na Katibu wake, Abeid Msingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles