KIPINDUPINDU CHAUA WATU 900 YEMEN

0
490

 

 

Sana’a, Yemen

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema watu zaidi ya 923 nchini Yemen wamefariki dunia kutokana na kipindupindu.

Kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa juzi na WHO,   watu wengine 124,000   wameambukizwa kipindupindu katika mikoa 20 ya nchi hiyo tangu mlipuko wa ugonjwa huo  Aprili mwaka huu.

Wizara ya Afya ya Yemen nayo imetoa wito kwa jamii ya kimataifa hasa Umoja wa Mataifa (UN) kutekeleza ahadi za kuwasaidia  watu nchini humo katika sekta ya afya   waweze kukabiliana na kipindupindu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here