25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kipindupindu chashika kasi Dar

Pg 3NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

MAAMBUKIZI ya ugonjwa wa kipindupindu yamezidi kushika kasi mkoani Dar es Salaam, baada ya idadi ya wagonjwa kuongezeka kutoka 34 hadi kufikia 43.

Ongezeko hilo limekuja ikiwa ni siku tano tangu kugundulika kwa ugonjwa huo, ambao tayari umesababisha vifo vya watu watatu.

Akizungumza na MTANZANIA, Dar es Salaam jana, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Dk. Azizi Msuya, alisema kutokana na ongezeko hilo, wamelazimika kutoa huduma kwa wagonjwa wote waliopo kwenye kambi ya Hospitali ya Mburahati.

“Mpaka sasa hatujapokea taarifa ya  mgonjwa wa kipindupindu aliyefariki dunia katika wilaya yetu… juzi tumewaruhusu wagonjwa wanne na jana tumeruhusu watatu,” alisema.

Alisema kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo, manispaa imejipanga kutoa elimu ya nyumba kwa nyumba kuhimiza usafi katika familia pamoja na kunyunyizia dawa sehemu za  mazalia.

Dk. Msuya alisema ni muhimu jamii itambue kuwa chanzo cha ugonjwa huo ni uchafu unaotokana na mazingira husika, hivyo haina budi kuzingatia usafi na kuepuka ulaji ovyo wa vyakula bila mpangilio.

Naye Muuguzi Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye ndiye msimamizi wa kambi ya Mburahati, Nusura Kessry, alisema kambi hiyo imezidiwa kutokana na wagonjwa wanaotoka katika vituo vingine kuhamishiwa kituoni hapo.

“Tuna wagonjwa 21, kati yao 10 wanatarajiwa kuruhusiwa kutokana na afya zao kuimarika. Tatizo kubwa linalotukabili ni ufinyu wa eneo kwa kuwa tuna uwezo wa kuhifadhi wagonjwa 16 tu.

“Kambi hii inatarajiwa kuwa kituo kikubwa cha wilaya na wagonjwa wote walioko hospitali za  Sinza na Mwananyamala watahamishiwa hapa,” alisema.

Akizungumzia uwapo wa vifaa tiba kwenye kambi hiyo, alisema mbali na ufinyu wa eneo na kuhitaji mahema hawana tatizo jingine.

Alisema kutokana na ongezeko la wagonjwa wanaohamishiwa katika kambi hiyo, ni muhimu kila mtu achukue tahadhari juu ya ugonjwa huo.

“Familia wanapogundua kuwapo kwa mtu mwenye dalili hizo, ni vyema kuwahishwa katika hospitali iliyo karibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles