23.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

Kipindi cha Take One cha Clouds chafungiwa miezi mitatu

Gigy-Money (kushoto) akiwa katika kipindi cha Take One
Gigy-Money (kushoto) akiwa katika kipindi cha Take One

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds na kukifungia miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na kituo hicho.

Kipindi hicho kilichosababisha kufungiwa kilikuwa mahojiano kati ya mtangazaji Zamaradi Mketema na Gift Stanford ‘Gigy Money’ kilirushwa Agosti 9 saa 3.00 usiku na kurudiwa Agosti 10 saa 7.00.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Method Mapunda, alisema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kukiukwaji kwa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,293FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles