27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, December 14, 2024

Contact us: [email protected]

Kipande cha bawa la ndege ya Malaysia iliyopotea chaonekana Mauritius

mabaki-ya-ndege

Kipande cha bawa la ndege chaonekana katika kisiwa cha Bahari ya Hindi cha Mauritius na inasemekana ni cha mabaki ya ndege ya Malaysia, imethibitishwa na maafisa wa Malaysia pamoja na Australia.

Awali, wataalamu wanaoendelea na utafiti wa ndege hiyo iliyopotea kutoka Ofisi ya maafisa wa Usalama wa Usafiriji ya Australia, waliokota kipande kingine cha bawa kwenye fukwe za bahari ya Hindi pwani ya Magharibi ya Australia.

Kwa kulinganisha namba zilizokuwepo kwenye ndege hiyo na zile zilizopo kwenye bawa lililopatikana, Waziri wa Usafirishaji wa Malaysia, Liow Tiong Lai amethibitisha kuwa ni yenyewe.

Uchunguzi unaoendelea kufanyika ndani ya Bahari ya Hindi kwenye eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 120,000 (maili 46,000), unatarajiwa kumalizika mwezi Disemba.

Wataalamu wa mambo ya bahari wanaendelea kuchunguza baadhi ya mabaki yaliyopatikana Tanzania na Kisiwa cha La Reunion, Ufaransa ili kuona kama itawasaidia kupata eneo li8ngine litakalowasaidi kuendeela kufanya utatifi wao wakuyapata mabaki yaliyosalia baharini.

Ndege hiyo ilipotea  Machi 8, 2014 ikiwa na abiria 239, ilipokuwa ikisafiri kutoka Kuala Lumpur, Malaysia kuelekea Beijing.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles