27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kipa Simba aumwa saratani ya mgongo

dhaira-2NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

ALIYEKUWA kipa wa Simba na timu ya Taifa ya Uganda, Abel Dhaira, amethibitika kuwa na ugonjwa wa saratani ya uti wa mgongo.

Kwa mujibu wa daktari wa klabu ya IBV Vestmannaeyjar ya nchini Iceland, anayodakia kipa huyo, ugonjwa huo ndio uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Dhaira aliyewahi kuidakia Simba msimu wa 2013/14, alianza kusumbuliwa na ugonjwa huo tangu Januari mwaka huu na baadaye kupelekwa Hospitali ya Nsambya ya Kampala nchini Uganda wiki sita kabla ya kurudi Iceland.

Baada ya kurudi mji wa Nordic uliopo  kwenye kisiwa hicho ambako ndiko yaliko makazi ya klabu yake, madaktari waligundua kuwa kipa huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani na si vidonda vya kawaida vya tumbo.

Awali kipa huyo alikuwa akilalamika juu ya maumivu ya vidonda vya tumbo  ambavyo alidai vilikuwa vinamfanya kusikia maumivu makali kwa muda mrefu.

Tangu mwaka 2013, Dhaira hakuweza kupangwa kwenye timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) kutokana na maumivu hayo, huku mashabiki wa timu hiyo wakiwa kwenye matarajio ya kipa huyo kurejea mapema kwenye kikosi cha timu hiyo.

Hata hivyo, kocha wa IBV, Bjarni Johannsson, alidai kusikitishwa na ugonjwa huo uliomtokea mchezaji wake na kuahidi kuwa pamoja naye kuelekea kwenye mchezo wa wiki ijayo.

Dhaira mara ya mwisho kuonekana kwenye kikosi cha IBV ilikuwa Oktoba mwaka jana, baada ya kuomba kupumzika kutokana na kusumbuliwa na afya yake.

Baadaye ilimlazimu kurejea nchini kwao ili kuitembelea familia yake iliyoko Kijiji cha Walukuba, mji wa Jinja, Uganda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles